"Aise mfunike blanketi vizuri asije akaumwa na mbu."

21:21:00 Unknown 0 Comments

Jamaa flani alikuwa na wasi wasi kuwa mkewe si mwaminifu akapanga safari feki.

Usiku akamtafuta rafiki yake wakamfumanie kwa ushahidi. Wakanyata na kufungua milango mpaka chumbani,jamaa na pistol tayari mkononi,ile kufunua blanketi kweli wakamkuta mkewe na mwanaume mwingine.

Jamaa kakasirika anataka kumtwanga risasi mwizi wake.

MKE:"Mume wangu subiri,huyu ndie mfadhili wetu, analipia ada ya shule ya watoto, ndie aliyefanya mpango ukapata kazi,ndie aliye nunua friji,home theatre,TV amelipia DSTV miezi sita,hata kodi ya nyumba sikukopa kama nilivyosema alilipa yeye."

MUME:"Aise mfunike blanketi vizuri asije akaumwa na mbu."

You Might Also Like

0 comments: