Kutoka kwa rafiki wa Fuledi

16:22:00 Unknown 0 Comments

Tangu nihitimu chuo ni mwaka wa tatu sasa, na nimekuwa nikihangaika kupata ajira bila matuaini na kuishia kufanya vibarua ambavyo bado havikuweza kukidhi mahitaji ya familia yetu na wadogo zangu wawili wanaosoma shule ya sekondari pamoja na mama yetu ambaye ni mgonjwa.

Baba alifariki na mama ni wa makamo na amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na kuathiri afya yake jambo ambalo mpaka sasa limemfanya ashindwe kuwa msaada kwetu na kututegemea sisi hasa mimi.

Ilinibidi nije mjini ili kuweza kupata koneksheni za kazi jambo ambalo liliishia kuwa gumu na la kukatisha tamaa kwa miaka yangu yote miliwi niliyokaa hapa dar. Hebu fikiria huna kazi lakini unatakiwa kumsaidia mama apate dawa na wadogo waende shule vyema(Yahitaji ujasiri na kujituma sana).

Sikuwa na jinsi zaidi ya mimi kumtegemea rafiki yangu ambaye yeye alibahatika kupata kazi na akawa akinipa msaada mkubwa sana. Wiki iliyopita nilimwambia adhma yangu ya kurudi nyumbani kuwa karibu na familia lakini moyoni lengo lilikuwa kurudi kijijini na kujikita katika kilimo na kazi za kujitolea kwani niliona nakuwa mzigo kwake kwani nami nilitaka nimpe nafasi ajijenge. Kiukweli alinikatalia na kunisihi nibaki ila mimi moyoni nikawa nilishamaanisha.

Juzi usiku nilijifungia chumbani mwangu na kumwambia MUNGU wangu,” Eeh MUNGU, wajua mahitaji yangu na wakati mgumu nilio na unaona jinsi nilivyohangaika. Sasa nimeamua kurudi nyumbani,ila naomba uwe upande wangu na kumsaidia mama na wadogo zangu wapate matunzo, kwani wewe ndiwe mtunzaji mkuu”

Baada ya salahii nililala, jana nilipigiwa simu na shirika moja la kimataifa ambalo niliomba kazi miezi miwili iliyopita na wakanifanyia usaili na kuniruhusu niondoke. Leo asubuhi nikaitwa na nilipofika pale nikapewa barua ya kuitwa kazini.

Wakati nikiwa bado na mshangao nikaona katika mambo makuu nitakayopewa ni bima ya afya ambapo sasa naamini mama atapata matibabu kwani naruhusiwa kuwaweka watu wanaonitegemea wa umri wowote wasio zidi wanne.Pia sasa kwa mshahara huu mkubwa nitakaoanza kuupokea naamini wadogo zangu watamaliza elimu yao bila shida.

MUNGU ni mwema na hamtupi mtu anayemtegemea na kumwita nakati za shida au raha.

You Might Also Like

0 comments: