Barua kwa rafiki:

20:00:00 Unknown 0 Comments

Kwako Rafiki

Ulikuja jana usiku kuniambia kuwa kwa sasa umefikia uamuzi wa kuomba kumpa talaka mkeo.

Jana usiku nilikusikiliza tu, lakini leo asubuhi nimeamka nikiwa na wazo jipya lenye habari njema na ya matumaini kwako.

Kwa zaidi ya miaka 5 nimekuwa nakutana na watu mbalimbali wa makamo ambao wao wamedumu katika ndoa zao kwa miaka 25 na zaidi ili kufahamu kuhusu Maisha yaa ya ndoa.

Kwa nyakati tofauti wote walisema Maisha yao ya ndoa yamepita katika zama tofauti zenye maumivu na faraja. Na zaidi ni kuwa kuna wakati hata iliwabidi wafikiri hata kuachana kwa muda ingawa hawakufikia uamuzi huo.

Lakini pia nilishawahi kuongea na wapenzi ambao wao waliamua kuachana kwa muda ili kutafakari kama bado wanafikiri wangeweza kuishi tena kwa pamoja wakiwa na furaha upya.Ingawa kila mmoja wao alionyesha hali ya kujutia uamuzi ule na kuona kama hakuivaa nafasi yake kama mme au mke kuzuia maamuzi yale.

Tumaini langu kwako ni hili, Jipe muda wa kufikiri na kutafakari kama kweli hayo yanakutoka moyoni au ni kutokana na hisia mbadala ulizonazo sasa.

Jipe muda wa kutafakari na baada ya hapo mkiachana nani ataweza kuja kuziba nafasi na asiwe na mapungufu?

Baada ya kutafakari hayo utaweza kuja na njia mbadala ya kuiokoa ndoa yako na kuweza kuishi tena Maisha ya furaha.

Wengi tumekuwa katika mahusiano yetu tukimezwa na maamuzi ya haraka bila kujua nini ningefanyika ili kuokoa mahusiano, na pia wengi tumechoswa na tabia za wapenzi wetu na tumekuwa na aibu ya kusimama nqa kuokoa maahusiano yetu dhidi ya kuharibika.

Kumbuka Shetani unayemjua ni bora kuliko malaika usiyemjua

Jioni Njema

Fuledi

You Might Also Like

0 comments: