Gazeti lazua balaaa
Fuledi alikuwa akisoma gazeti lake na
wakati huo huo mtoto wake alikuwa
akimsumbua kila mara na kumfanya ashindwe kutuliza akili yake kkatika gazeti lake.
Ili kumfanya mtoto awe bize Fuledi
akalichukua gazeti na kulichana sehemu yenye ramani katika vipande vipande ili
mtoto aunganishe upya.
Fuledi alikuwa na imani kuwa mtoto Yule
angeitumia siku nzima kuunganisha ramani ilewakati yeye akipata nafasi ya kukaa
vyema na kumaliza kulisoma gazeti lake bila kuwa na usumbufu wa aina yoyote ile.
Lakini mtoto Yule ndani ya dakika
chache alikuja akiwa kaiunganisha ramani ile kwa urahisi kabisa …….Fuledi alipomuuliza mbona umetumia muda
mchache hivi? Mtoto alijibu,
“Oh….Baba, kulikuwa na picha ya sura ya mtu upande wa
pili wa ramani katika gazeti……Nikaipanga
upya sura ile na kugeuza upande wa pili
ramani ikawa imekaa vyema.”
Mtoto akakimbia nje na kuendelea kucheza na wenzake huku akimwacha Fuledi akiwa katika
mshangao.
Funzo:
Kumbuka
kuna upande wa pili wa furaha katika kila jaribu gumu unalolipitia katika dunia
hii. Na utapatwa na mshangao kuona jinsi ilivyorahisi kutatua tatizo lako
linalokusibu sasa..
Jambo la msingi ni kuwa na matumaini
katika mafanikio
0 comments: