Huwezi kuruka hapo
Siku moja kundi la vyura lilikuwa likisafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Vyura hawa wakati wanaruka juu ya mabanzi ya miti kwa bahati mbaya vyura wawili wakaangukia kwenye shimo refu.
Wale vyura wengine wakaja na kulizunguka lile shimo na kuwambia wale vyura wawili kwa jinsi shimo lile lilivyo refu hawataweza kutoka na hakuna msaada wowote wa kuwatoa wale vyura.
Lakini wale vyura wawili walizidi kujitahidi kuruka juu ili waweze kutoka ndani ya lile shimo , lakini wenzao wakazidi kuwaambia waache maana wasingeweza kutoka mle shimoni.
Wakaendelea kujitahidi kuruka bila mafanikio huku wenzao wakiwaambia kuwa waache tuu na baadae chura mmoja akakata tamaa kuanguka chini zaidi na kufa lakini yule mmoja akaendelea kujitahidi kuruka.
Aliendelea kuruka pamoja na wale wa nje kumkatisha tamaa na baadae akajikuta katoka nje ya lile shimo.
Alipotoka mle shimoni wenzake wakamuuliza, "kwani ulikuwa hutusikii kuwa usingeweza kutoka?"
Yule chura akajibu kuwa, " Nina matatizo ya kusikia sauti zikiwa mbali, nikiwa kule chini sikuwa nawasikia ila kila milivyonyoosha mikono nikadhani mnanipa ishara ya kuwa nizidi kuruka nitatoka"
Funzo
Ili kujitoa katika hali uliyonayo unatakiwa kujituma bila kusikiliza nini watu wanasema hasa kwenye mambo ya kukatishana tamaa.
Ni vyema kuziba masikio kwa baadhi ya mambo na kuweka akili katika nini ufanyacho ili kufikia malengo yako
0 comments: