Ilibaki kidoogo tuu iwe tayari
Mimi ni kijana wa miaka 35 na nimekuwa na tabia ya kupenda sana totozi hasa wale wa vyuo. Sijajua hili tatizo lina sababiswa na nini.Hivi majuzi nilipata bahati ya kukutana na dada mmoja mrembo sana sana na huyu yeye akaniambia ni mfanya biashara toka kule Mbeya na hupenda kuja Dar kwa ajili ya shopping na pia kujiliwaza.
Basi kijana mie kama kawaida yangu siku mwacha aende zake bila kumweka mtegoni na baada ya hapo akaniambia nimcheki jioni maeneo ya sinza alikofikia ilituweze kujadiliana mawili matatu.
Jioni ile bila kukosa nilijisogeza na kumkuta yupo kwa room nami nikaingia na kuketi kitandani na kuanza mazungumzo mawili matatu huku tukitupia kinywaji kabla ya kuanza kulimega tunda la katikati. Mmmmh kweli binti hajambo maana kwa muda mchache nilisahau maswahiba ya kidunia kwa kweli.
Siku ya pili aliondoka na kurudi zake jijini mbeya huku akinipa mwaliko wa kwenda kumtembelea nami nikamwahidi kuwa lazima nitaenda hasa nikikumbuka ile makitu ya jana yale.
Tukawa tunaendelea kuchati kupitia FB na juzi nikaamua kupanga safari ya ghafla kuja hapa mbeya kumtembelea mtoto mzuri tena kwa suprize, nikachukua usafiri wa hewa mpaka songwe na kisha kuingia town na kutafuta hotel na kupanga kisha nikampigia mtoto naye hakusita ndani ya dakika chache alikuwa kaingia si wajua tena mbeya masualaya foleni kama zile za dar sahau.
Sikuamini usafiri alioingia nao maana binti yule alikuja na usafiri sio chapa mjapani bali chapa England kwa wale wapenzi wa magari wanajua nazungumzia nini.Baada ya furaha na mabishano ya hapana pale mtoto akanisihi niondoke hotelini nikalale kwakwe kwani pale yeye hana mme tukakubalina na kuwasha gari kisha kutokomea.
Ebwana weee yule binti suprize ya pili aliyonipa ni jumba analoisha ni tamu na la kisasa na kwa binti kama yule ni balaa kumiliki zile mali ati.
Basi baada ya kushangaa na kumpa hongera zake akanitembeza sehemu mbalimbali za jumba lake na jiji la mbeya usiku ule kabla ya kurudi zetu kwa ajili ya mapumziko.Baada ya kuoga na hadithi za hapa na pale ikabidi kijana nianze kukamia kilichonisafirisha kwa raha zangu.
USiku wa saa tisa nikiwa na mausingizi nikaamka na kwenda zangu bafuni ile narudi si nataka kuweka taulo kwa bahati mbaya nikaufungua mlango wa kabati lake la nguo......Basi niliona jitu la ajabu limenitolea macho kabla hata sijajua nini cha kufanya likataka kunidaka shukuru Mungu nikaanguka chini na kujivuta haraka mlangoni na kutoka kwa spidi ya ajabu ile kufungua mlango wa nje yule mlinzi alikuwa kalala.
Sikugeuka nyuma nilitimua mbio mpaka tax moja iliyokuwa ikielekea uelekeo wangu kusimama pembeni yangu na dereva kunipa lifti, sikuongea neno mpaka asubuhi ya jana baada ya kushtuka nipo mahali nisipopajua kabla ya yule dereva kutokea na kunikumbusha alikonikuta.
Baada ya kumsimulia dereva mkasa mzima alinicheka na kusema kaka usivamie miji hovyo,yule mama anatumia utajiri wa Tunduma (aka ule wa kujambia chungu) na ushukuru maana leo ungekuwa kafara. Maana kashaua waume zake zaidi ya wawili.
Duh ilinibidi niachie kaushuzi, kwani sikuamini na mpaka sasa bado kichwani naona maluweluwe na sijui nini kinaendelea zaidi ya kumshukuru Mungu pamoja na dereva tax huyu.
Kesho nategemea kurudi Dar nikiwa na nia moja tu ya kuokoka na kumrudia Mwenyezi Mungu wangu.
Jamani tusiwavamie wadada wa mjini/facebook bure na tukumbuke sio kila king'aacho ni dhahabu. Leo hii mwenzenu ningeweza kuwa mahala pengine pasipo na facebook.
Asanteni na naomba maombi yenu katika safari yangu ya kurudi Dar ambako napenda kukuita "Home Sweet Home"
0 comments: