Jinsi misumari ilivyomaliza hasira za Fuledi

01:16:00 Unknown 0 Comments




Kulikuwa na kijana mmoja aliyeitwa Fuledi, Kijana Fuledi yeye alikuwa ni mtu mwenye hasira sana na alikuwa hawezi kuzizuia.

Baba Fuledi akamwita mwanae na kumwambia “ mwanagu Fuledi chukua mfuko huu wa misumari pamoja na nyundo. Na kila utakapokuwa na hasira chukua nyundo na msumari mmoja kasha pigilia kwenye fensi”.

Siku ya kwanza Fuledi alipigilia misumari 37 katika fensi ile,Baada ya wiki akajikuta misumari inazidi kupungua na taratibu ikaanza kwisha kabisa ikipigiliwa katika fensi ile.
Fuledi akatambua kuwa kumbe ni rafisi kutuliza hasira kuliko kupigilia misumari kwenye fensi ile.

Mwishowe ikafika siku Fuledi akawa hana hata chembe ya hasira kabisa.

Akamwambia baba yake na baba akafurahi sana na kumwambia fuledi aende akaitoe ile misumari na kila siku autoe mmoja mmoja ili asiwe na hasira kabisa.

Siku zikasonga na siku moja Fuledi akaja na kumwambia baba yake kuwa misumari yote imetoka kwenye fensi.

Baba akasema “Umefanya vyema Fuledi, Mwangu, ila angalia mashimo ya misumari katika miti uliyoipigilia kwenye fensi. Fensi hii itabaki na mashimo hayo ya misumari milele. Unavyosema vitu ukiwa na hasira huacha vidonda kama unavyoviona kwenye miti ya fensi hii.”


Unaweza mchoma mtu kisu na kukitoa lakini haitajalisha utasema pole mara ngapi, lazima kovu litabaki hata apone vipi huyo mtu.

Funzo

Jaribu kuhakikisha unaimudu hasira yako kwani unaweza fanya jambo sasa na ukalijutia miakayako yote.

You Might Also Like

0 comments: