Kuishi na binadamu kazi kweli kweli
Kulikuwa na masichana mmoja kipofu ambaye alijichukia kwa kuwa haoni.Lakini pia aliwachukia watu wote kasoro kijana mmoja ambaye alikuwa mpenzi wake kwa sababu muda wote alikuwa jirani yake akimpa faraja na matumaini.
Binti huyu alimwahidi kijana yule kuwa kama siku moja angefanikiwa kuona tuu basi kitu cha kwanza ni wao kuoana.
Siku moja kuna mtu akaamua kutoa macho yake ili binti yule aweze kuona vitu mbalimbali vilivyomo katika dunia hii pamoja na yule mchumba wake. Mpenzi wake akamuuliza, “Sasa umeweza kuona je utanioa?”
Yule binti alishtuka kumwona kijana yule kuwa nae ni kipofu, Bilakufikiri binti yule akakataa ombi lakuolewa na yule mchumba kipofu. Kijana yule akaondoka huku machozi yakimtoka
Siku chache baadae yule dada alipokea voicemail (ujumbe wa sauti) kutoka kwa yule kijana ukisema:
“Tafadhali naomba yatunze macho yangu.”
Funzo
Hivi ndivyo jinsi ubongo wa binadamu unavyosahau mambo na kubadilika. Ni wachache ambao hukumbuka mema uliyowafanyia na kuwa nawe katika vipindi vigumu vya mapito yako. Hata ukijitoa vipi ni wachache watakao uthamini mchango wako.
0 comments: