Nawapenda wazazi

11:27:00 Unknown 0 Comments




Penseli: Samahani.

Mfuto: Kwa nini? Mbona hujafanya kosa lolote

Penseli: Nisamehe,kwa sababu unaumia kila mara kwa kufuta makosa yangu. Kila nikosapo huwa karibu kuyafuta makosa yangu.Na kila unapofuta makosa yangu sehemu yako huisha na huumia kwa ajili yangu.

Mfuto: Ni kweli na uko sahihi, Lakini wala usijali. Kumbuka,Nilitengenezwa ili kufuta makosa yako, Na ninatakiwa kuyafuta makosa yako kila mara na kwa gharama yoyote ile, Na ninaelewa kuwa siku moja nitapoteza kabisa kutokana na kazi hii. Ila nina furaha kwa kazi yangu. Hivyo basi usiwe na wasiwasi na punguza hofu.

Funzo

"Wazazi wetu ni kama mifuto/Ufutio, sisi watoto ni kama penseli. Wazazi wetu kila mara wapo kwa alijili ya kuyafuta makosa yetu. Hujivunia kuwa wazazi wetu na katika kutufanya tuwe safi (kutulea vyema) huzeeka na mwishoe hufa. Penda wazazi wako kwa moyo wako, wape upendo na kuwajali kwani wao ndio wamekulea na kukutetea mapaka unafikia hatua uliyopo sasa"


You Might Also Like

0 comments: