Njemba ikazimia
kuna njemba ilikuwa inamkong'ota nakumdunda waif wake vibaya sana mpaka yule
mama akawa anaiogopa hii njemba vibaya
sana.
kuna siku hii njemba iliumwa ikaenda hospitali
na ikatakiwa kupeleka mkojo, njemba ilirudi
home na ikatia mkojo kwenye kichupa na
kukiweka pembeni ya kitanda. wakati
anatandika kitanda kwa bahati mbaya yule
mke wa hii njemba akaumwaga ule mkojo, kwa
kuogopa mkong'oto na kipigo cha njemba
akaamua atie mkojo wake yeye, halafu
auchune kama hakukutokea kitu, bikozi
angesema kaumwaga angeng'olewa meno yote
kwa kipigo.
siku ya pili njemba ilichukua mkojo na
kupeleka hospitali ,madaktari walionekana
kuwa na tafrani na mshangao flani na kuja
kuoneshana ile njemba ikiwa imekaa pale
inasubiri majibu. na hatimae daktari mkuu
akaiita hii njemba chumbani na mambo
yakawa kama yafuatavyo.
daktari: ndugu,una uhakika huu mkojo ni wa
kwako?
njemba:(:ikajibu kwa jeuri na hasira) ushaona
mkojo nimeuleta mimi halafu unauliza kama
wa kwangu?, wako wewe basi!! aaaargh
daktari::(baada ya kuona njemba ni jeuri na
yeye akaamua kuijibu kwa kejeli) hongera
ndugu una ujauzito wa miezi miwili! .
njemba ilizimia.
0 comments: