Mr Rwegoshora

13:40:00 Unknown 0 Comments


Mr Rwegoshora alimaliza LLB yake hapo Mlimani na kuamua kurudi kwako BKB kusaidia wateja
ambao wana matatizo ya kisheria.
Siku ya kwanza wakati ndio amefungua ofisi yake,alimuona kijana mtanashati anakuja kuelekea
ofisini kwake.
Hapo ndipo alipoanza kunyanyua mkono ... wa simu ya TTCL, wakati anajizungusha kwenye viti
virefu.
Wakati kijana alipokaribia Rwegoshora alionesha kumkaribisha wakati anaongea na
simu,alisikika akiongea ''No.no, no, Absolutely no, You tell those clowns in New York that I
won't settle this case for less than one million. (pause)
Yes, yes . The Appeals Court has agreed to hear that case next week, I'll be handling the primary
argument and the other members of my team will provide support. Okay. Pliz dont forget to tell
the State Prosecutor that I'll meet with him next week to discuss the details."
Yule kijana ametulia tu anamuangalia bwana Rwegoshora anajinyonganyonga kwamuda zaidi
dakika 5.
Baada ya kumaliza kuongea na simu,bwana Rwegoshora alielekea kwa huyu jamaa. ''Samahani
sana, kwa kukupotezea muda wako, unajuatena kazi zetu hizi unaumiza kichwa sana, kama
unavyoona tena mwenyewe hapa, yaani nikobusy sana, ninapokea simu mpaka nimechoka
mwenyewe. enh by the way, what can i do for you?
Jamaa alijibu. '' Mimi ni mfanyakazi wa TTCL, nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani
haipo hewani'

You Might Also Like

0 comments: