Nina kila sababu ya kujibu ni kwa nini nawatakia siku njema wanawake wote duniani...... soma
Siku moja jioni
mtoto fuledi alimfuata mama yake jikoni
akiwa ana andaa chakula cha jioni na kumpa mama yake kajikaratasi kadogo ambako
fuledi alimwandikia
Mama Fuledi
alifuta mikono yake na kukichukua kile kikaratasi ambacho kilisomeka hivi:
Kwa ajili ya
kukata nyasi nakudai : TZS 5000
Kwa kusafisha chumba changu wiki hii nakudai : TZS 4000
Unavyonituma dukani nakudai : TZS 1000
Kukaa na mototo ukiondoka : TZS 2000
Kutupa takataka nakudai : TZS 3000
Kusoma kwa bidii nakudai : TZS 5000
Kusafisha sehemu ya baba kupaki gari nakudai: TZS 1500
Jumla alidai: TZS 21,500
Kwa kusafisha chumba changu wiki hii nakudai : TZS 4000
Unavyonituma dukani nakudai : TZS 1000
Kukaa na mototo ukiondoka : TZS 2000
Kutupa takataka nakudai : TZS 3000
Kusoma kwa bidii nakudai : TZS 5000
Kusafisha sehemu ya baba kupaki gari nakudai: TZS 1500
Jumla alidai: TZS 21,500
Mama akasimama
pale baada ya kulisoma lile karatasi na baadae akatabasamu na kumpokonya peni
na kuandika kitu kisha akampa fuledi asome.
Mama aliandika
hivi:
Kwa miezi tisa
niliyo kubeba tumboni mwangu huku ukiendelea kukua:
Sitakudai
Kwa siku zote usiku ambazo sikulala kukubembeleza na kukupambia kitanda:
Sitakudai
Kwa miaka yote niliyokulea na ukanipa wakati mgumu na machozi juu yako:
Sitakudai
kwa nyakati zote za usiku ambazo sikulala nikikuuguza ili upone:
Sitakudai
kwa kila mdoli, chakula, nguo na hata kelele zako:
Sitakudai
Mwanangu Fuledi, Hata ukiongeza upendo wangu kwako:
Sitakudai
Fuledi baada ya
kumaliza kusoma huku macho yakijawa na machozi alisimama na kumwambia mama
“Mama, Kutoka moyoni nakupenda.” Na kisha akachukua lile karatasi na
kuandika kwa kimombo “PAID IN FULL”.
Funzo:
· Hutajua
umuhimu wa wazazi wako mpaka utakapo kuwa mzazi.
· Uwe
mtu wa kutoa kuliko kupokea kama wafanyavyo wazazi wetu
· Kuna
mengi wazazi wametupa zaidi ya fedha.
·


0 comments: