Hamadi Fuledi anakutana na Anna maeneo ya Coco beach
Fuledi: Hi mrembo, unaonekana kunivutia na ile nakuona tu mapigo yangu ya moyo yakasimama kwa dakika chache na kisha kurudi kwa kishindo yaani shwaaa!! .. naweza kuongea na wewe??
Anna: Yep wala usijali.. jina lako nani?
Fuledi: Hahahaaa watu wanapenda kuniita people Eng. 'Fuledi' ila nitafurahia kama wewe ukiniita Eng. Dr Fuledi.. na wewe nomino yako ni ipi?
Anna: Unasema?!??.
Fuledi: Yeuwiiiii! Unaitwa nani mrembo?
Anna: ohooo Annastacia
Fuledi: Jina zuri sana, heri kwa boyfriend wako kuwa na mtu mzuri kama wewe..
Anna: ..Asante ila tumeachana naye hivi karibuni..
Fuledi: Oooh, hili ni jambo la kuhuzunisha sana bibie, samahani na nini kilikuwa chanzo cha nyie kuachana?
Anna: Alianza kwa kunipeleka Dubai kwa ajili ya mapumziko na hivi majuzi kanipeleka Afrika ya Kusini kwa ajili ya shopping....
Na sasa hebu fikiri yaani anataka kunipeleka shopping eti Mlimani City????????
Nikaona ameanza kunidharau au ana wanawake wengine nikaamua kuachana nae
Fuledi: Unajua niko busy kidogo kama vipi mida .. Nimefurahi kufahamiana na wewe..


0 comments: