Jumamosi mbaya kuliko zote maishani mwangu

15:36:00 Unknown 0 Comments



12.00 asubuhi

Niliamka nikiwa na uchovu wa kazi kwani jana
yake tulikesha ofisini na kuja kulala saa nane na
nusu, nikajitundika bia nap kulala.Asubuhi hii
niliamka nikiwa na uchovu wa ajabu

1:00 Asubuhi

Baada ya kuoga nikaweka samaki wangu motoni
kwa ajili ya supu na kisha nikawasha laptop
yangu na kufungua facebook yangu na kuona
friend request ya binti mmoja mzuri na
kuiaccept.

2:00

Nikapata text kutoka kwa mrembo
niliyemwasepti akidai ananifahamu sana nami
nikachati nae sana kwani kila text ilinifanya
niisubiri majibu okwa hamu na kutokana na
uwezo wake wa kuunda maneno matamu.
3:00
Akaniambia mtaa aliopo nami nikashangaa kwani
haikuwa mbali sana na nyumbani kwangu
nikamtania kuwa natamani kumtoa out.

4:00

Baadae mabishano yakafika ukingoni na
kukubaliana tukutane sehemu na tuongee kwa
ajili ya kuifurahia weekend.

5:00

Nikawasha gari langu baada ya kujiandaa na
kisha kuanza safari ya kunako miadi yangu na
yule dada.

6:30

Nikakutana na binti yule na kisha taratibu
tukazama kwenye gari na kuanza safari kuelekea
sehemu mmoja nje ya mji ambako kuna hotel
moja maarufu na ya kitalii.

7:00

Tukiwa spidi mara gari moja likatupita kwa kasi
na baadae likaimega na kukaa katikati na
kutufanya tusimame, mara wakashuka jamaa
wakiwa wamevaa mask na kunitoa garini
kunifunga vitambaa nisione na kisha kunibeba
juu juu mpaka garini mwao na kisha kuondoka
na gari langu na yule binti kuviacha pale.
Nikafika na kuingia nyumba mmoja na kuwekwa
kwenye chumba kimoja chenye baridi kali na
kisha kufunguliwa kitambaa na kuona pale tupo
wawili tu na mama mmoja ambaye nae
kafunikwa kichwa kizima.

8:00

Kuangalia saa yangu muda huo ilikuwa ishatimia
saa nane kamili na bado tupo wawili na muda
huo wote nikiwa na hamu na shauku ya
kumfahamu yule mama.

9:30

Baada ya muda wa saa moja na zaidi pale ndani
mara mlango ulifunguliwa na akaja kijana mmoja
aliyefunikwa uso na kumtoa kile kitambaa yule
mama na kisha kuondoka.

Mama yanguuuuuuu, sikuamini kile nilichokiona
kwani niliduwaa kwa zaidi ya dakika kadhaa, yule
mama ni mke wa mtu na ni miezi miwili tuu
imepita tangu aninunulie gari ninalolitumia na
nimekuwa na mahusiano naye ya kimapenzi kwa
muda sasa.

Wote tuliangaliana bila ya kuongea na mama
alionekana kama alipigwa sana na anashindwa
kuongea.

4:00
Baada ya kukaa mle ndani kwa dakika kadhaa
mara alitokea tena yule kijana akiwa na
kitambaa usoni mwake ili asionekane na
mkononi kashika kitambaa pia, akanifunika na
bila kusema kitu kisha akanitoa na akanipeleka
kwenye gari na kuondoka.

Tulizunguka na gari kwa muda mrefu na baadae
wakanishusha sehemu bila kuongea na
kuondoka.

1:00

Kuangalia saa ilikuwa ni saa moja kamili ya usiku
na kucheki mitaa nikagundua nipo nje ya
nyumba yangu na kuingia ndani nikaona gari
yangu imepaki nje na funguo zipo ndani yake
nikazitoa.

Nikaingia ndani mwangu nikamalizia kiporo cha
samaki wangu na kisha nikaanza kula bia nikiwa
na hofu juu ya tukio hili.

Mpaka sasa sijui imekuaje???? Je yule mke
aliendaje pale, na yule binti alitumwa na mme
wa yule mama au laah na je nini kitaendelea
baada ya hapo au nifanyaje sijui na
nimechanganyikiwa.

Natamani kulirudisha gari na kukimbia mji
Comment ushauri na share wengi wamsaidie
Facebook majanga

You Might Also Like

0 comments: