Njia rahisi ya kumpa fedha mbongo na akashindwa kuzitumia milele

13:52:00 Unknown 0 Comments



Mzee mmoja wa kizungu mwenye asili ya kimarekani aliwasili katika kijiji kimoja kimoja kiitwacho UWEMBA kilichopo kusini mwa Tanzania.

Mzee huyu akafika katika nyumba ya mzee mmoja ambaye alikuwa maskini wa kutupwa na kuomba hifadhi ya kukaaa pale kwa muda wa miezi kadhaa ili aweze kumaliazia utafiti na uchapishaji wa kitabu chake.

Familia ile maisha yalibadilika kwa muda huo wakila na kutoka out kila mwisho wa juma na kula vinono huku kila kitu kikienda vyema na kila walichohitaji kama matumizi ya familia mgeni alitoa.

Maisha yakawa mazuri na kila mwanafamilia akamshukuru yule mgeni na Mungu pia kwa kuwaletea mgeni mwenye baraka kama yule.

Miezi minane baadae yule mzee wa kizungu akawa ameshafanikiwa kumaliza kuandaa na kukichapisha kile kitabu chake.

Akaandaa tafrija ya kushtukiza ya kuwashukuru wale wenyeji wake na kusema hana cha kuwashukuru zaidi ya kuwapa zawadi ya kitabu kimoja ili nao wakisome.

Wenyeji wale walifurahi na kuwa na matumaini kuwa asubuhi ya pili yakr pia akiwa anataka kuondoka angewapa tena pengine gari lile na fedha nyingi kwani walishajifunza kuwa mgeni wao ni tajiri wa kutupwa.

Siku ya pili yake asubuhi mgeni aliondoka bila kuacha chochote zaidi ya kile kitabu na kuondoka zake.

Wenyeji walichukia na baba akakitupia kitabu ndani kwake na kuendea kuumia kwa mgeni wao kuwaacha watupu ingawa aliamini kuwa kuna siku labda wangetumiwa kitu.

Siku zikaenda bila ya matumaini na familia ile ikazidi kuwachukia wageni na hata walipotumiwa barua za salamu kutoka kwa yule mgeni wao kamwe hawakujibu kama ishara ya kuumizwa.

Ikapita miaka zaidi ya 18 yule babu baada ya kuona kimya akaona apange safari ya kuja kutembelea mbuga za wanyama hapa Tanzania ili pia aweze kwenda kuwasalimia wale wenyeji wake waliompa msaada akiandika kitabu chake miaka kadhaa iliyopita.

Alipofika pale alishangazwa kuona ni maskini zaidi ya alipowacha...

Akawauliza jamani kitabu changu mlikisoma kweli????????

Wote wakajibu ndio na nikizuri sana sana.... 

Akaomba kama wanacho akione kama wamekitunza vyema.

Baba akaingia ndani na kukichukia na akampa mgeni wake.

Mgeni akakichukua na kukifungua baaada ya kugundua hakikuwahi kufunguliwa wala kusomwa yaaani kama alivyokiacha.

Kufungua ndani ikaanguka bahasha ndogo katikati ikiwa na maneno

" MAFANIKIO YETU DAIMA HUJIFICHA PALE TUSIPOPADHANI AU TUNAPOPADHADHAU......DAIMA TAFUTA MAFANIKIO HATA KAMA YAMEFICHWA USIPOFAHAMU... ASANTENI KWA KUNIKARIMU"

Ndani ya bahasha kulikuwa na cheki yenye thamani ya TZS 50,000,000/- 

Mzee na wanawe wakaishia kulia na kuomba mzee awasamehe .

RAFIKI

Soma sana kwani ni kwenye vitabu na hata kwenye mitandao ambako utakuza maarifa yako na ukiyahamisha na kuyatumia kuboresha kazi zako huko utapata mafanikio zaidi ya cheki ya mzee.

whatsapp 0713317171

You Might Also Like

0 comments: