*SOMA HADITHI YA KWELI YA BINTI MWANAMITINDO WA KITANZANIA*

13:43:00 Unknown 0 Comments



Dada mmoja aitwaye Doc aliyekuwa na kipaji na hamu ya kuwa mwanamitindo ndoto zake zilikatishwa kutokana na changamoto mbalimbali na misukosuko iliyomkabili yeye kwa wakati huo.

Akazidi kumwomba Mungu aijalie familia yake unafuu wa changamoto hizo na hatimaye aweze kuifikia malengo yake na kuwa mwanamitindo.

Akaja rafiki yake mmoja aliyekuwa akiishi nje ya tanzania na kumpa zawadi ya simu yenye kamera bora na ya kisasa kumfanya Doc aweze kupiga picha za kisasa na kuzihariri tayari kwa kupeleka sehemu mbalimbali ili watu waone kazi zake.

Siku moja akaona tangazo kwenye mtandao wa facebook  likielezea juu ya kampuni mpya ya mitindo iliyowataka watu wakapeleke picha zao na mshindi apate mkataba wa kazi

Kwa kuwa ofisi hazikuwa mbali dada yule akatembea kwa miguu kuelekea huko, akiwa katika uchochoro mmoja vibaka wakamvamia na kuipora ile simu ambayo ilikuwa na picha zake zote.

Dada alilia huku akirudi nyumbani na kusema Mungu nilikuomba unipe njia nawe ukanipa lakini leo tena vibaka wamechukua na ndoto imefia hapa..... Uko wapi Mungu wangu??????????

Akarudi nyumbani na kushirikiana na familia kuomboleza, na maisha yakarudi yale ya mwanzo bila kuwa na matumaini ya kuifikia ndoto yake tena.

Wale vibaka wakaenda kuuza ile simu kwa jamaa mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya mitindo na wakuvutiwa na picha zile za doc kwenye ile simu.

Wiki chache baadae dada yule alitafutwa kupitia baadhi ya majina ya kwenye ile simu yake iliyoibiwa baada ya jitihada za yule kijana na kurudishiwa simu yake.

Akisaini mkataba wa kufanya kazi na kampuni hiyo na sasa kapata mkataba na kampuni moja ya mitindo yenye makao makuu jijini mbeya iitwayo GREEN team photogenic na sasa ni mtu mweye maisha mazuri na familia yake inafurahia jitihada za mwanao.

Mungu hutujibu maombi yetu kwa namna tofauti hivyo zidi kuomba na kumtumaini yeye ukimshirikisha katika mipango yako.

Comment Amen kama unaamini uwepo wa neema na  nguvu za Mungu katika kufanikisha mambo yetu na mipango yetu maishani  na kisha share

Like Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: