Hii ni ajabu na kweli..... Ona imani za watu juu ya jumatatu

06:58:00 Unknown 0 Comments

Tukiwa shuleni tuliamini ukianza jumatatu kwa kuchelewa au kuwa na adhabu shule basi wiki hiyo yote itakuwa ni ya adhabu kwako.

Watu wengi huamini kama ana duka na akaanza kwa kukopesha basi siku nzima biashara yake itakuwa ni ya mikopo au kutokuwa na wateja wanunuzi walio wengi.

Pia ni watu wengi ambao wao huamini kuwa siku au wiki nzuri ni ile ianzayo kwa mafanikio na furaha maana huishia ikiwa na mafanikio yenye furaha zaidi.

Watu wengi zaidi pamoja na mimi huamini siku mpya, wiki mpya au mwaka mpya ambao mtu huanza kwa kujikabidhi kwa Mungu huwa na mwisho mzuri zaidi wenye mafanikio yenye furaha endelevu zaidi.

Je wewe uko upande upi?

Sala ndogo kwako

"Eeh Mungu wangu, nakukabidhi siku yangu ya leo na wiki hii mpya, naomba nipe furaha na manikio kuanzia nyumbani, kazini, darasani na katika kila nitakachokigusa kiwe na kibali kutoka kwako na hatimaye nionje furaha na mafanikio ya mipango yangu chini ya ulinzi wako huku ukiniepusha katika mitego ya yule mwovu.. AMEN"

You Might Also Like

0 comments: