Maskini ya Mugu!!!!!!!!!!! Kaka afia usingizini wiki chache kabla ya harusi yake....Vilio vya Tawala... Mbeya hapashikiki

21:01:00 Unknown 0 Comments



Jioni moja wapendanao wawili Gwantwa na Salva walikutana katika hotel moja maarufu sana kwa ajili ya kuipanga safari ambayo wangeianza siku ya pili yake mapema sana.

Wapendanao hawa walitaka kuzitumia likizo zao ambapo kila mmoja aliomba kazini kwake ili wapate muda wa kusafiri na kufurahi pamoja katika sehemu mbalimbali kama kumbukumbu ya mwisho ya uchumba wao kwani zilibakia wiki tano tuu wafunge harusi.

Baada ya kuridhika na mpango wa safari yao ambayo wangeianzia katika hifadhi ya taifa ya Ruaha na kisha kwenda kuimalizia Serengeti baada ya kwenda Zanzibar na baadhi ya mikoa ya kusini, wote kwa pamoja wakaiita "SAFARI MUHIMU YA KUKUMBUKWA YA WAPENDANAO WAWILI"

Wakarudi majumbani kwao kwa kuwa walikuwa wakikaa sehemu tofauti na kisha wakafungua group la whatsapp na kulipa jina lile na ku-add marafiki ili kila sehemu watakapofika wakutane na marafiki wa sehemu ile na kufurahi nao na kweli group likaanza kwa chati nzuri na ukaribisho wa kutosha.

 Wakapigiana simu na kukumbushana kuamshana asubuhi na kuwa Salva angewahi kwenda kumpitia Gwantwa ili waende uwanja wa ndege tayari kwa safari kisha wakalala.

Asubuhi Gwantwa akawahi kuamka akajiandaa na kusubiri Salva aje ampitie na safari ianze. Ulipita muda bila Salva kutokea, Gwantwa akapiga simu ikawa inaita haipokelewi, akatuma meseji kote whatsapp, facebook, na kwenye simu akawa anaonekana online ila hajibu chochote.

Kwa hasira Gwantwa akatuma meseji za kumlaumu lakini hakujibiwa pia, wazo la haraka likamjia ili wasichelewe ampigie mpangaji mwenzake na Salva ambaye akagonga mlango bila mafanikio.

Muda huo tayari Gwantwa alishafika pale akiwa na mabegi yake na walipojadili wakaona ni bora wavunje mlango ingawa Gwantwa alijua Salva atakuwa na binti mwingine ndani.

Walipofanikiwa kuvunja mlango, maskini ya Mungu!!!! walikutana na mwili wa Salva ukiwa umelala kitandani kwani alikufa kifo cha ghafla akiwa usingizini na mambo yote yakabadilika na kuwa si suala la safari tena ya furaha ila sasa ni jambo moja tu la kuwasiliana na ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi huku Gwantwa akipelekwa hospitalini baada ya kuzimia.

Rafiki wa fuledi,

Gwantwa na Salva walipanga mambo kibinadamu na hawakumshirikisha Mungu kwani nilitegemea hata walipofika nyumbani wangesema tusisahau kumshukuru Mungu kwa kufanikisha kulipanga hili na kisha kabla hata ya kufikiria kuamshana salama wangekumbushana kuombeana na kuiombea safari yao.

Je wewe ni mara ngapi umepanga au kufikiri kitu bila ya kumshikisha Mungu wako???

Ni nani kati yetu anayeweza kusema ameamka salama kwa nguvu zake mwenyewe?
Nimeuliza hivi kwani muda sio mrefu nimebahatika kukutana na baadhi ya watu wakijisifia kuwa wameamka salama kwa  kwa nguvu zao.

Sijui wao wana miungu ipi zaidi ya Mungu ambaye anastahili kushukuriwa kwa upendo wa kutuhurumia na kutuvusha siku hii  salama tena kwa mapenzi yake.

Ni wangapi wamekufa kwa fitina, ajali, magonjwa na hawajaiona siku hii?

Lakini sisi twaamini ni kwa mapenzi yake Mungu wetu ndio maana leo tupo salama.

Naamini wengi walitamani kuiona siku hii wakiwa na mipango mingi ya maendeleo au sisi pia tulitamani kuwa nao na ikashindikana.

Kaka, dada na rafiki yangu kama umeweza kuamka na kuusoma ujumbe huu jua ya kwamba Mungu anakupenda na uzidi kuomba ulinzi wake kwa siku ya leo, kesho, na mwaka huu pia.
Comment neno "AMEN" kama unasababu ya kumshukuru Mungu wako na kuomba afya njema na mafanikio na ulinzi katika mwaka huu

share ujumbe huu na like Tabasamu na Fuledi

Ujumbe huu umeletwa kwenu kwa hisani ya marafiki wa fuledi

You Might Also Like

0 comments: