"mwanangu unayemuulizia amekufa miaka miwili iliyopita" haya ndio majibu niliyopewa asubuhi, wakati binti huyu nimecheza naye club ijumaa

20:34:00 Unknown 0 Comments

Ilikuwa ni ijumaa ya furaha sana na kama unavyojua mtu uliyekaa muda mrefu maisha yakiwa yamekushika huna mbele wala nyuma mpaka unazushiwa majina ya mzee wa kizinga Yule anakuja……..duh ilikuwa tabu kweli kweli Maisha yale ,lakini ijumaa hiyo nilikuwa na furaha sana kwani nilikuwa nimeshafanikiwa kupata kazi na nimeshapokea mshara wangu wa kwanza na upo saafi ndani ya akaunti yangu.

 Niliingia chumbani, nikatupa vifaa vyangu vya ofisi nikaingia bafuni nikapata maji nikarudi na kutupia viwalo vya ukweli na baada ya hapo nikawasha gari mpaka kwa Nene.

 Nene ni mmoja kati ya marafiki zangu wa karibu sana na kipindi chote alikuwa akinipa sapoti sana hasa wakati nafanya michakato ya kupata kazi, kwani niliitumia ofisi yake na kompyuta zake kutuma maombi sehemu mbalimbali bila ya yeye kuwa na kinyongo mpaka pale nilipopata kazi. Hivyo nikaona ni vyema tutoke wote kwa siku ile kama moja ya kulipa fadhila kwa msaada wake.

 Nilimkuta kasha jiandaa na wote kwa pamoja tukawasha gari mpaka bar na kazi ikaanza mwendo wa ndovu kwa kwenda mbele. Ilipotimia mida ya saa tano wote tukakubaliana twende club.

 Club ilikuwa imeshapamba mtona DJ alikuwa akiifanya vyema kazi yake tulicheza cheza kidogo kabla ya kuingia binti mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Noreen. Duuh!!!!!!! nikasema kama noma na iwe noma leo lazima motto nimuweke ndani ya himaya yangu hasa ukizingatia jinsi alivyonikonga kwa mavazi aliyoyapiga na zaidi alinipagawisha jinsi alivyoweza kucheza,kiukweli nilidata. 

 Tuliendelea kucheza na baadae bia zikaendelea mpaka pale Nene aliponiambia kachoka hivyo nikamrashi home nami nikamrudisha Noreen kwao .Ingawa nilimshusha njia panda hakutaka nifike kwao kwani hakutaka kuwashtua home kwa mungrumo wa gari lakini ilinibidi nimpe sweta langu ili ajisitiri kwa baridi kali usiku ule kwa makubaliano kuwa siku ya pili yake nikamchukue ili mambo mengine ya fuate hasa ukizingatia nilikuwa na hamu naye baalaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 Tuliachana pale nami kikarudi home na kulala ila kila nilipotaka kulala zilinijia picha mbalimbali za Yule mtoto zaidi ni jinsi kwa mda mchache alivyoweza kunipa changamoto. Sikufikiri hata siku kama ningeweza kummiliki mtoto mtamu aka mzuri kama Yule.
 Siku ya pili niliamka nikiwa mchovu na baada ya kufanya mambo mawili matatu nikajiandaa kwenda kumtembelea Noreen. 

 Niliendesha gari mpaka nyumba aliyonielekeza jana yake usiku na baada ya kufikapale nikagonga na kuingia ndani, nikapokelewa na binti mmoja.

 Cha kushangaza ni baada ya kumwambia Yule binti kuwa namuulizia Noreen, Yule binti alianza kulia na kumwita mama yake, duuh jasho likaanza kunitoka na kuhisi labda Noreen ni mke wa mtu? Nikaendelea kujiuliza maswali mengi mpaka mama mtu akaja.

 Mama mtu akaniambia mwanangu unayemuulizia amekufa miaka miwili iliyopita na kaburi lake halipo mbali, ikanibidi niwasimulie mkasa mzima,na baada ya hapo wakanipeleka kuona kaburi,nilishangaa kuona lile sweta nililompa Noreen lipo juu ya kaburi..Kidogo nizimie lakini shuzi kali niliyoitoa ilinifanya nione aibu na kukaa kimya.

 Mpaka sasa siwataki wanawake wa club kwani bado sijui alikuwa jini au nimechezewa mchezo

Hebu soma nawe uone ushauri wa marafiki HAPA

You Might Also Like

0 comments: