Wachache sana wanaweza kuwa na wewe hata kama utapitia safari za aina hii............
Marafiki wawili waliamua kujiajiri na kuanzisha kampuni ya pamoja ambayo ilijihusisha ya masuala ya uuzaji wa magari.
Walipendana na kuzidi kushikamana mpaka siku moja wakaja kuishuhudia biashara yao ikizidi kuwa kubwa na kuwavutia wateja wengi zaidi.
Walimshukuru Mungu kwa bahati hiyo na kuuzidisha uhusiano wa familia zao na mapenzi baina ya familia hizi mbili yakaongezeka maradufu na kufanya kuwa familia za mfano pale wilayani kwao.
Miaka ikazidi kwenda na mafanikio yakazidi kuwa mikoni mwao nao wakamshukuru Mungu wao kwa bahati hiyo.
Miaka michache baadae mmoja wao hali yake ikaanza kusumbua kutokana na maradhi yasifofahamika na akaugua kwa muda mrefu na wakizunguka sehemu mbalimbali kutafuta tiba bila ya mafanikio yoyote yale.
Mke wa yule mme mgonjwa akawa akimfuata yule rafiki wa mme wake ambaye wanafanya biashara kwa pamoja japo ampe fedha kidogo za kumsaidia kumuuguzia mgonjwa kwani wao akaunti yao ya familia ilikuwa imepukutika kabisa.
Pamoja na kuwa alikuwa akipigwa kalenda na rafiki pamoja na kupewa maneno yasiyo ya busara yaliyomshangaza kuwa ni vipi rafiki kabadilika, mara hii aliumia na kulia baada ya rafiki kumpa SANDA na kusema ikamsaidie kupunguza bajeti wakati wa mazishi ya mme wake maana hataweza kupona kamwe.
Mama aliondoka huku akiwa analia na kuomba kwa Mungu kuwa amponyeshe mme wake na kumfanya awe hai na kushuhudia jinsi rafiki alivyomgeuka mapema.
Wiki moja baadae yuke rafiki aliyetoa sanda alipatwa na ajali mbaya na kuvunjika uti wa mgongo na sasa yeye amekuwa kilema, yaani ni mtu wa kubebwa na haja zote hujisaidia hapo hapo alipo.
Yule rafiki mgonjwa alitoka hospt na sasa ni mzima na anaendelea na kazi kama kawaida.
Funzo
Rafiki kabla hujafa hujaumbika hivyo thamini na kuwajali wale wote wenye matatizo bila kuwakejeli au kuvicheka vilema vyao au hali walizonazo kwani nao hawapendi.
Na daima kumbuka kuwa rafiki wa kweli kwa marafiki zako katika nyakati zote, yaani nyakati za jua na mvua.
Siku njema na kama umeipenda andika SAWA na kisha share
like Tabasamu na Fuledi
0 comments: