Baba mwenye nyumba ananiharibia ndoa
Kwa bahati mbaya nimefukuzwa kazi na maisha yameanza kuwa magumu sana kwangu na familiayangu.
Hali hii ikapelekea hata kulipa pango iwe tatizo na hivi karibuni nilikutana na baba mwenye nyumba
akaniambia sasa nisilipe ila nikiwa na kazi nitaanza kumpa kwani sasa kanisamehe.
Na wiki jana kamwajiri mke wangu katika duka lake kubwa la kuuzia madawa ya binadamu.
Mbaya zaidi ni kwamba mtaani kuna tetesi kuwa mke wangu anatembea na baba mwenye nyumba
akiwa kazini.
Na baada ya uchunguzi nimebaini kuna ukweli.
Naombeni mnishauri nini nifanye maana nashindwa kuamini kama mke wangu ambaye nimezaa nae watoto wawili anaweza nisaliti kwa changamoto hizi....

0 comments: