ha ha ha ha pesa kiboko
JAMAA alikuwa kagombana na mkewe, hatimae akamwambia mkewe kwa ukali, "Unajua nimechoka sasa haya kusanya nguo zako na......"Kabla hajamalizia sentensi simu ya mkewe ikalia, kumbe alikuwa ni baba mkwe. Basi mzee akaanza kuongea na binti yake baada ya salamu, na katika kile kimya Jamaa kasikia mkwewe akisema, "
Aise binti nimebahatika nimeuza ile nyumba yangu ya Moshi sasa nimeona niwatumie milioni 20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio, haya mwambie ntampigia kesho, kama ana mradi mwingine nimpe fedha kidogo".
Baada ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa akamuuliza 'Ehe ulikuwa unasema umenichoka nikusanye nguo na nini?' Jamaa kwa upole akajibu, " Nilikuwa nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue"
0 comments: