Jamaa atoa ushuhuda wenye maumivu, "Nilitembea uchi ili cheo kipande kazini lakini mke akatibua"
Haki ya nani tena mambo yaliniwia magumu na kuwa nje ya uwezo wangu hasa ukizingatia wife pale nyumbani alishaanza kukata tamaa na maisha tuliyoishi kwa muda huo.Mbaya zaidi pamoja na jitihada zote nilizozionyesha pale kazini lakini sikupata bahati hata ya kusingiziwa kwenye kupandishwa cheo au hata kuwa mfanyakazi bora.
Nikaanza kuona kama vile hali sio nzuri na uvumilivu ukinishinda kabisaaaaa.
Dan alikuwa mmoja wa washauri wangu hivyo akanipa wazo la kwenda kwa sangoma na kuniahidi kuwa baada ya hapo lazima nitwpandishwa cheo na hatimaye kuja kuwa boss pale ofisini.
Mganga akanipa masharti ya kuwa ni lazima nitembee uchi kutoka nyumbani kwangu mpaka ofisini na kuwa wala nisijali kwani kila mtu ataniona nimevaa nguo.
Na akasisitiza kuwa kama mtu akishtuka au kunitazama kwa mshangao basi nijue kuwa naye anatumia nguvu za giza kama nilizonazo mimi.
Siku ya pili yake asubuhi mke wangu akaniandalia nguo na mimi sukuvaa nikaondoka nikiwa uchi ila sikuona mtu akinishangaa.
Nilipoingia kwenye daladala kuna mama mmoja akapiga kelele ingawa hakusema chochote zaidi ya kunishangaa nami nikajikausha nikijua ni muumini mwenzangu.
Ofisini hakuna aliyeshtukia zaidi ya secretary ambaye alitimuka mbio na dereva wetu mmoja nikajua kuwa hao ndio wenye tunguli pale ofisini.
Nilivyorudi nyumbani mke akaniuliza mbona hukuvaa nguo nilizokuandalia? Nikamjibu kuwa nilivaa nyingine naye hakushtuka nikatulia.
Siku ya pili yake nikiwa ofisini ila nikiwa na nguo nikaitwa kwa boss na kupewa barua ya kuwa sasa nimekuwa meneja wa pale.
Nikafurahi na kuona dawa zimefanya kazi, nikaanza kukitumikia cheo changu kipya kama meneja nikiwa na mbwembwe nyingi.
Wakati huu mke wangu akawa ameshangazwa na kitendo cha kupandishwa kwangu kazi hivyo akaanza kuomba sana akihisi ni nguvu za ajabu kwa kuwa elimu yangu ilikuwa ndogo
Wakatio huo mimi nikatafakari na kuona kuwa nilistahili nafasi kubwa zaidi hivyo nikamtembelea mganga wangu tena na wakati huu akanipa mtihani mpya.
Mganga akasema natakiwa kumchukua mtoto wangu mchanga nimlaze makaburini kuanzia saa sita usiku mpaka alfajiri na mke wangu asigundue.
Nilirudi na kila nipotakiwa kumchukua mtoto nikamlaze makaburini kama alivyosema mganga nilipitiwa na usingizi kutokana na sala za mke wangu na kujikuta dhamira ikinisuta.
Nilijaribu kwa takribani wiki kadha kila nikimshika mtoto mke wangu anashtuka na najikuta nasutwa na dhamira yangu.
Mganga akanipa jambo la mwisho la kuifanikisha dhamira yangu kuwa nitatakiwa ni atanipa uwezo wa kuwaona watu wakiwa uchi kama walivyozaliwa wakija ofisini mwangu pale kazini kaa masharti ya kutocheka.
Siku ya kwanza tuu nikiwa pale ofisini akaja jamaa mmoja aitwaye bonge na alijifanya mjanja sana alipoingia nikashangaa kuona nae kavaa hirizi nyingi na mbaya zaidi sehemu alikozifunga ni matata hasa kwenye dushelele.
Nikajisahamu na kucheka huku nikizuga nasoma meseji na huo ndio ukawa mwisho wa ajara na maisha kuwa magumu na hatimaye kuamua kuokoka.
Nawe kama waamini ndumba katika kazi zako jua huna lolote zaidi ya kuitwa mpuuzi.
Kama hauamini katila nguvu za giza kupata mafanikio share ujumbe huu na kisha comment "looser' hapa
0 comments: