KISA KITAKACHOKUFANYA ULIE KAMA UNA MOYO WA HURUMA
Kengele ya kutoka darasaniiligongwa, wanafunzi wa shule ya
msingi wakaanza kutoka
madarasani huku wakifukuzana
wengine wakipiga kelele ilimradi
shwangwe tu.
Ilikuwa mara yangu ya kwanza
kufundisha shule za hatua hiyo.
Ilikuwa ni shule ya serikali.
Jicho langu liliangukia katika sura
ya msichana mdogo, nguo zake
chafu. Alikuwa analia.
Alikuwa peke yake na hakuwa na
yeyote wa kumbembeleza. Mimi kama mwalimu sikutaka
kujisogeza karibu naye sana.
Kwanza nilikuwa mgeni.
Nikaachana naye.
Siku iliyofuata tukio kama lile
likajirudia. Msichana yuleyule
wakati ule uleule wa kutawanyika,
alikuwa analia sana. Mwishowe
aliondoka huku akiwa analia.
“Mbona mwenzenu analia?”
nilimuuliza mwanafunzi mmoja.
“Huyo ni mama kulialia..”
alinijibu huku anacheka.
Haikuniingia akilini hata kidogo
kuwa yule binti analia bila
sababu.
Siku ya tatu nikaanza kujiweka
karibu naye.
Muda wa mapumziko nilimwita
nikamnunulia chai, alikuwa
ananiogopa na hakutaka
kuniangalia machoni.
Sikumuuliza lolote juu ya tabia
yake ya kulia lia kila anaporuhusiwa kurejea
nyumbani.
Hata siku hiyo pia alilia vilevile.
Wenzake wakawa wanamzomea.
Akili yangu iligoma kuamini kuwa
binti yule analia bila sababu.
Kwanini alie wakati wa
kutawanyika tu?? Hapana si bure.
Nikaendelea kujiweka karibu
naye. Mkuu wa shule akafikishiwa
taarifa kuwa nina mahusiano ya
kimapenzi na yule mtoto.
Moyo wangu na Mungu pekee ndio
walikuwa mashahidi. Nilikosa cha
kujibu. Nilijaribu kujiweka mbali naye lakini moyo ulinambia kuwa kuna jambo natakiwa kulijua.
Nikaendelea kuwa karibu naye.
Hatimaye mkuu wa shule
akanisimamisha kufundisha pale
kwa tabia yangu ya kufanya
mapenzi na mwanafunzi.
Nilijitetea lakini sikueleweka.
Nikamwachia Mungu……
Licha ya kusimamishwa kazi,
niliendelea kufuatilia nyendo za
yule binti aliyeitwa Janeth.
Kila alipotoka shule nilimvizia
njiani na kumnunulia chakula,
kisha tunazungumza kidogo.
Aliponiamini kama kaka yake
ndipo nikajieleza dukuduku lake.
“Janeth…” nilimuita.
“Bee kaka ….” Aliitika huku
akinitazama.
“Nyumbani unaishi na wazazi.”
“Ndio naishi na mama..baba huwa
anasafiri safari.”
“Mama yako ana watoto
wangapi?”
“Mama yangu alikufa….alikufa
nikiwa mdogo hata simkumbuki”
Alijibu kwa sauti ya chini.
“Kwa hiyo unaishi na mama
mdogo.”
“Ndio.”
“Unampenda mama mdogo?”
Swali hili likaikatisha furaha ya
Janeth. Akaanza kulia, alilia bila
kukoma, Janeth alilia kwa
uchungu hadi nikajisikia vibaya.
Nilimbembeleza kisha
sikumuuliza tena.
Siku zikaenda bila kumuuliza
chochote..
Baada ya siku kumi, ilikuwa siku
ya michezo pale shuleni, hivyo
hapakuwa na masomo.
Janeth alichelewa kuja shule,
nilimngoja uwanjani, hadi
alipofika majira ya saa nne.
Nikamwambia twende kunywa
chai.
Siku hiyo nilimpeleka mbali
kidogo, tukanywa chai, kisha
tukakaa mahali palipokuwa wazi.
Nikaleta tena mjadala mezani.
Ni kuhusu maisha ya Janeth.
Alikataa kabisa kusema lolote,
nilimshawishi sana.
“Usiogope mimi ni kaka yako.”
Nilimpooza.
Janeth badala ya kusimulia
akaanza kulia tena.
“Ataniua mama nikisemaaaa”
alilalamika.
Nikambembeleza hatimaye
akanieleza jinsi anavyonyanyaswa
na mama yake.
“Mama hanipendi hata kidogo,
ananipiga na kuninyima chakula,
hapendi nije shule, vyombo
tunavyotumia usiku hataki
nivioshe usiku na hataki niwahi
kuamka asubuhi, nikiamka
natakiwa kufanya kazi zote,
kufagia uwanja, kudeki nyumba,
kuosha vyombo kisha ndipo nije
shule. Baba akiwepo anajidai
kunijali sana…”
Alijieleza.
“Ni hayo tu Janeth….niambie kila
kitu.”
“Akijua ananiua alisema….”
“Kwani amewahi kukutesa vipi..”
Ni hapa Janeth alivyozungumza
huku analia kilio ambacho
hakitatoka masikioni mwangu
kamwe.
Siku moja, alichelewa kuamka,
ilikuwa siku ya mapumziko.
Mama yake alipomwamsha,
aliitika na kupitiwa usingizi tena.
Mama aliporejea mara ya pili,
alikuwa na mti mkavu, alimpiga
nao kichwani na popote pale
katika mwili, alipoona hiyo
haitoshi akamvua nguo,
akausokomeza katika sehemu za
siri, aliuigiza hovyohovyo, ukuni
huo ulikuwa wa moto.
Yeyote mwenye moyo wa nyama
ajifikirie ukuni wa moto
ukazamishwa sehemu za siri za
mtoto wa darasa la sita.
Nilitokwa machozi.
Nikawahi kujifuta hakuona.
“Baba yeye alisemaje….”
“Baba ni mkali na hapendi
kunisikiliza na mama aliniambia
nikiambia mtu ananiua mara
moja.” Alijibu kwa huzuni.
“Nikija na dada yangu tunaweza
kukuona ulivyounguzwa..”
“Ndio…” alinijibu.
Sikutaka kulaza damu nikampigia
simu rafiki yangu wa kike.
Nikamuuliza kama yupo kwake,
alikuwepo.
Nikaongozana na Janeth.
Tukafika, Janeth akatoa nguo zote.
Ilihitaji moyo wa kiuaji sana
kutazama mwili wa Janeth mara
mbilimbili.
Alitisha, hakika alikuwa
ameunguzwa vibaya na vidonda
vilikuwa havijapona vizuri.
Dada yule alishindwa kujizuia
alimlazimisha Janeth twende kwa
mama yake amkabiri na kumpa
kipigo. Nikamzuia.
Hata mimi nilikuwa na hasira kali.
Lakini sikutaka kuiruhusu ifanye
kazi.
Nikachukua kamera, nikampiga
picha Janeth katika yale makovu.
Mbio mbio nikaenda polisi, kituo
cha haki za watoto nikaelezea
mkasa ule huku nikishindwa
kujizuia machozi.
Nikawaonyesha na picha.
Tukaongozana nao hadi nyumbani
kwao Janeth.
Mama yule akakamatwa bila
kutarajia.
Nilitamani kumrukia nimng’ate
lakini haikuruhusiwa.
Sheria ikafuata mkondo. Janeth
akaanza kupokea tiba.
Yule mama akahukumiwa kwenda
jela miaka sita..hadi sasa yupo
jela.
Mume wake alitozwa faini kubwa
kwa kosa la kutofuatilia
maendeleo ya mtoto wake kiafya……..
Mimi nilirudishwa kazini, kwa
heshima kubwa. Heshima ya
kumkomboa mtoto.
***Akina JANETH wapo mtaani
kwako…..usiwaangalie na
kuwaacha tu…hebu jaribuKUWA
SAUTI YAO… .
hawawezi kusema…
hebu sema badala yao…….wanalia
kisikie kilio chao…….
KAMA UMEGUSWA NA MKASA
HUU COMMENT "PONA HARAKA MTOTO JANETH" NA SHARE NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI ZAKO ILI WAONE
0 comments: