Msome kijana mtanzania ambaye alinusurika kunyongwa kisa mapenzi

20:25:00 Unknown 0 Comments

Nilichungulia kupitia ule mwanya pale dirishani na kuona gari moja aina ya verosa ikiingia pale hostel na robo saa baadae mpenzi wangu Vivian akiwa na rafiki yake wa karibu Nancy wakaingia katika lile gari na likaondoka.

Ilinuchukua zaidi ya saa kufikiri na baadae nikafuta machozi ambayo yalianza kuninyemelea na nikaondoka zangu pale na kwenda zangu mitaani nikiacha baaadhi ya mabinti wanking'ona kwa chinichini kuwa bila hela huwezi miliki mtoto mzuri.

Niliumia sana nikafikiri miaka miwili tuliyokaa pamoja na jinsi alivyokuwa akitumia fedha zangu na sasa eti kwa kuwa nimefulia ndio anaanza kunidharau na kunidhalilisha hivi.. Na kama vipi si angekuwa mkweli tukaachana?

Nikaanza kuona hasira zinazidina kila siku napunguza spidi ya darasani jambo amablo hata wenzangu wakanishauri niachane nalo. kweli niliachana nalo ingawa kila nilipomwona Vivian akiingia kwenye lile gari la yule mzungu nikaumia sana.

Jumapili moja nikamwomba nancy aniitie Vivian na kuandaa sehemu moja nikae na kuongea nae kwa masaa kadhaa ingawa neno nililoambulia ni kuwa hajisikii tena kuwa na mimi hana tena mshipa wa upendo.

Nikamuuliza kama kuna sehemu nimekukosea niambie kwani nimejitahidi kukupenda na tulipendana sana tukiwa na ahadi zetu kibao lakini sasa hapa chuoni kumegeuka kuwa na story moja tu ya mimi na wewe kuachana na wewe ukiwa na mme wako.

Nakuomba hata kama nimekukosea na hutataka tuwe tena wapenzi basi tuwe tuu marafiki na huyo jamaa kama inawezekana uwe unaonana naye huko nje ukija hostel huku uko naye uondokapo hostel hugeuka na kuwa na mada moja ya kuniponda mimi sasa inanipa wakati mgumu.

Akaniangalia toka chini mpaka juu akadai usiniingilie katika mambo yangu nitafanya nitakavyo. niliumia kwa kweli na kuanza kufanya utaratibu wa kuhamia mtaani lakini kabla ya kufikia mwisho nikamshirikisha rafiki yangu mmoja.

Akaniambia nisiwe mjinga na kuamua kushindwa kijinga jinga, hivyo akaniambia kama nina kitu chochote ninacho cha kuweza kummwaribia niseme... nikagoma kwani sikuona kama ingekuwa na tija yoyote zaidi ya kuniletea madhara.

Siku chache baadae rafiki yangu akaja na wazo kuwa kwa nini tusimwaribie Vivian ili nae aumie kama navyoumia mimi? Maana muda mwingi nilikuwa mnyonge na ile hali ikawa ikimfanya rafiki yangu kunichukia sana.

Wazo lake likawa ni kama mimi nilishawahi kumpiga picha yoyote vivian akiwa uchi au yeye kama anazo kwenye simu. Mimi sikuwanazo kwa kuwa sikuwa napenda kukaa na picha kama hizo kwenye simu au hata kuthubutu kumpiga picha hizo.

Kilichobakia ikawa ni kumtumia rafiki yake Nancy ambaye akaniambia kuwa picha zipo nikamlipa hela na picha zile nikazihifadhi nikisikiliza maelekezo ya rafiki yangu.

Rafiki yangu akaniambia sasa kitu cha kwanza ni kutengeneza akaunti feki ya fesibuku na kisha kuziweka picha na baada ya hapo zianze kusambaa kutoka kwenye akaunti hiyo na kisha kwend akwenye blogs.

Wazo lile nikalipenda kwani wakati huo ubongo wangu ulitaka kisasi tu na kuona Vivian akigalagala kwa kulia na  kwa aibu kama mtoto mdogo, akishindwa kula na hata kuiona shule chungu na hata afukuzwe tu.

Mpango ukakamilika na harakati zikaanza na  ninakumbuka ilikuwa ni jumatatu moja majira ya saa nne nikaona mabinti pale hostel wakitoka mbilo kwenda nje.. 

Sikutaka kwenda maana sishabikihi umbea lakini kelel na mabishano yakazidi na nikaona niende maana kila mtu alikuwa akienda huko.Kufika pale nikaona watu wamzunguka mtu na nilipojaribu kupenyeza macho nikakuta ni Vivian akiwa kaanguka na ana damu tumboni zikimtoka na kabla ya kujua nini kinaendelea ambulance ikaja na kumchukua na baadhi ya watu wakamshindikiza.

Wazo la kwanza lililonijia nikajua lazima damu zile zitakuwa zimesababishwa na ugomvi kati ya Vivian na yule mzungu wake. Nikajivuta mpaka chumbani kwangu ambako nikaichukua simu yangu iliyokuwa kwenye charge na kumpigia rafiki yangu ili kumpa mkanda mzima.

Tukafurahi na kukutana bar moja nje ya hostel na kupata bia zetu tukijua sasa dada ndio moto unamwanza laba mzungu kaona zile picha maana zilishaanza kusambaa kwa kasi.

Nancy alituona akitokea hospitali, akaja pale haraka na kusema "mmefanya nini sasa" Vivian kapigiwa simu na baba yake na baadhi ya ndugu wameona vile picha kwani nyie mlimpa nani?

Nikakumbuka kuwa nancy tulimdanganya kuwa zile picha nitakaa nazo mimi kwani namkumbuka sana vivian, nancy akaendelea kuongea kuwa Vivian kajichoma kisu cha tumboni ili afe kwani ilikuwa ni aibu kupigiwa simu na ndugu zake.

"Na pia yeye kakuhisi wewe ndio umefanya hivyo sasa sijui itakuaje wakijua na mimi ndio nilitoa namba hizo nimeishiwa nguvu hapa shemeji", aliongeza maneno hayo nancy.

Muda huo zile bia tano nilizoziweka kichwani kwa fuaha nikaziona zikiishia kichwani na akili kuja. nikamuuliza  rafiki yangu kaka tufanyeje maana sasa ushahidi utaonekana au?

Akaniambia wala usijali tulitupia computer ambayo sio yetu hivyo hatutashikwa sisi hata wakifuatilia IP Adress.

Tukiwa tumekaa pale twajadiliana mara tukasikia king'ora cha gari bila kufikiri ni cha gari la polisi au ambulance tulikimbia tukielekea nyuma ya hosteli na kisha kutokomea mtaani.

Nikaanza kuona sasa kama ule uhuru wangu wa mtaani ukinitoka na muda huo zikaanza kuingia message kutoka kwa marafiki zikisema, kaka umemuua vivian kisa kusambaza picha zake kwenye mitandao...... nikaizima simu hiyo na kuwasha simu yangu yenye laini nyingine na ilivyowaka tu ikaingi sms ya VIVIAN iliyotumwa masaa mawli nyuma ikisema, " NAKUSHUKURU KWANI NAJUA NI WEWE TU ULIYEZITOA PICHA HIZO ILI MIMI NIAIBIKE, NA KAMA KUNA BAYA UNALIPANGA KWANGU BASI LIKURUDIE..ANSANTE"

Mungu wangu!!!! nikaona kama aliandika hiiyo basi ni ushahidi tosha wa kuniweka hatiani. nikamwangalia rafiki yangu na nancy nikawa sina la kusema zaidi ya kulia.

Nancy akasema kuwa anakumbuka simu ziko bwenini hivyo tukawahi kwenda kuziangalia ili pengine tufute ule ujumbe, tulifanikiwa kuzikuta na tukafuta ule ujumbe na kisha kufuta picha zote online na kuamini sasa hakuna kesi.

Baadae tukaitwa kwenda ukumbi mkubwa na kuambiwa ya kuwa Viviani alifariki muda mchache baada ya kupelekwa hosptitali kutokana na damu nyingi iliyotoka kwenye jeraha.

Wiki moja baada ya mazishi walikuwa jamaa wawili na kunichukua mpaka kituo kikuu cha polisi na kunifanyia mahojiano.. nikiwa pale nikaonyeshwa picha za VIVIAN na hata zile meseji na moja kwa moja nikaonekana ni mtuhumiwa namba moja.

Machozi yakaanza kunitoka na kujutia uamuzi nilioufanya kwa shinikizo la rafiki yangu na kuwa sasa kesi yote ni yangu.Nikapandishwa kizimbani na baada ya muda muchache nikagundua kila ndugu na rafiki wameniacha na kwa kuwa nilikuwa sina hata ubavu wa kumweka wakili basi kesi ile ikanikalia kooni.

Siku ya hukumu nikaambiwa kuwa nitahukumiwa kunyonywa kwa kuchomwa sindano yenye sumu.

Siku ilipofika nikaletewa mchungaji nikakaa nae na kuongea nae na kumwambia kuwa siku hiyo ningependa kabla ya kuuawa nile Ugali dagaa na kachumbali chakula nilichopendelea sana kula nikiwa na viviani na pia na soda moja ya kopo.

Nikaletewa na baada ya kula nikawekwa kwenye kiti tayari kwa kunyongwa.

Muda ulipotimia nikaongonzwa sala ile na kisha sindano ile ikawa imeruhusiwa nikawa naona maumivu makali kwa mbali mkojo ukaanza kunitoka kwa kasi kuashiria ya kuwa ndio nakata roho kabla ya kushtushwa na kibao kumbe nilikuwa nakojoa kitandani usiku......

Ndoto kama hizi sizipendi..

Duuuuh

Shame on me





You Might Also Like

0 comments: