SHERIA 12 MUHIMU ZA MPIRA WA MIGUU WAKATI TUKIWA WATOTO.

10:41:00 Unknown 0 Comments

1. Dogo mnene lazima awe Golikipa.

2. Mwenye mpira ataamua nani acheze na nani asicheze.

3. Penati itatokea tu pale mchezaji akiumia sana na kutoka damu.

4. Mechi itaisha kama kila mchezaji atakua amechoka.

5. Hakuna free kick, kitu kama icho hakipo kwenye mechi zetu.

6. Hakuna Refa, mchezaji anaweza kuzunguka na mpira ata nyuma ya goli.

7. Ukichaguliwa mwishoni ujue uwezo wako ni mdogo kuliko watu wote uwanjani.

8. Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufUata mpira ukitoka, au kutungua mpIra endapo utanasa kwenye mti uku wakisubiria mchezaji aitwe nyumbani kwao na wao wapate nafasi.

9. Mwenye mpira akikasirika, mechi ndo itakua imefika mwisho.

10. Inaruhusiwa kubadili golikipa kama penati ikitokea na baada ya penati golikipa anaweza kuendelea yule wa mwanzo.

11. Yule mtaalam wa soka huwa hakosi namba ata siku moja.

12. Mwenye mpira huwa hatolewi ata akicheza vibaya.

You Might Also Like

0 comments: