CONDOM imeniponza sasa familia imenigeuka

22:58:00 Unknown 0 Comments



Jana nikiwa ofisini asubuhi alikuja rafiki yangu akataka nimuazime gari ana safari ya kwenda sehemu na angeirudisha jioni kabla sijatoka ofisi.

Nikaona poa tu kwani ni best yangu na kweli akairudisha mishale ya saa 10 jioni.hapohapo ofisini. Kidume nikaondoka kurejea nyumbani na kupitia Sokoni kwa ajili ya maandlizi ya Sikukuu ya kuzaliwa ya mke wangu na leo hatukwenda kazini.

Leo wakati maandalizi ya mahunjumati yamepamba moto na nimealika marafiki zangu wawili waje tujumuke nao kama ilivyo ada, mara waifu akaingia ndani akasema kuna kitu muhimu kimekosekana hivyo nimpatie funguo awahi Sokoni kukinunua.

Nikampa na kumkumbusha juu ya kufungua boneti kucheki system za kawaida za gari kabla hajaondoka.

Baada ya muda nikiamini kuwa ashaondoka, mara akarejea na kulala kitandani na kunitupia fungua za gari. Sijaelewa kinachoendelea hivyo nikawa namdadisi kulikoni.

Akanijibu kamalizie na zile kondomu zako mbili zilizobaki, nikazidi kushangaa kwamba simuelewi, vipi kwani?

Nikatoka nje na kuelekea liliko gari, Hamadi! Nikakuta Kondomu 6 juu ya kiti cha abiria na 4 kati ya hizo zimetumika ila ziko kwenye kipakti lakini zinaonekana kirahisi tu, na inavyoonyesha amezitoa katika kisanduku cha kwenye Dash-Board ya gari ambako ndipo kwenye key ya kufungulia Boneti.

Nikazidi kuchanganyikiwa na harakaharaka likanijia wazo la kumpigia yule rafiki yangu, mpaka sasa simu yake haipatikani, na mapishi hapa yamesimama na hakuna linaloeleweka.

Mchango wowote wa ushauri plz!

Na myakague magari yenu pindi mnapoowazima marafiki zenu!

like before Tabasamu na Fuledi 

You Might Also Like

0 comments: