Rushwa ya ngono inaepukika

04:38:00 Unknown 0 Comments



Ndio kwaanza nilikuwa nimekabidhiwa kazi katika
kampuni ya Tabasamu na Fuledi Inc kama meneja wa utawala, na sikuwahi kupata uzoefu sehemu yoyote ile zaidi ya hapo nilipoanzia.

Kiukweli hali ya pale kazini ilikuwa tata kwa upande wa wanawake hasa ukizingatia ni kampuni ya matangazo na sanaa hivyo
vishawishi havikuniisha kwa jinsi kila binti alivyokuwa akionyesha kunitaka ila mimi nilizidi kuwa mgumu.

Kazi zilisonga na nakumbuka mkurugenzi wangu bwana Fuledi akishirikiana na Nasa walinikubali
na kunipa usaidizi wa karibu sana kila nilipowahitaji na kunifanya kuwa meneja bora niliyependwa na kila mfanyakazi na kuwaletea
mabadiliko chanya.

Siku moja nikiwa ofisini majira ya saa nne alitokea binti mmoja mrembo sio tu wa umbo ila
kila kitu kwake kilionekena swaaafi bila ya kasoro yoyote ile sio tuu machoni mwangu ila ni kwa
mwanaume yoyote yule hapa duniani bila ya kujali tabia, hali, rangi wala utajiri.

Binti akaniambia kuwa anahitaji kazi na kuwa alituma maombi kwani kuna kazi tulitangaza na
kuwa hajaitwa mpaka sasa.

Sikutaka kumweka sana ofisini nikamwambia kuwa tulishafanya usahili na kuwa sasa tumeajiri
hivyo hakuna kazi.

Binti yule akaa pale akilia kwa muda kisha akainua kichwa na kuniambia, "Meneja naomba
unipe kazi nitakupa chochote utakacho"

Kiukweli nikapigwa na butwaa na kujiuliza kwa muda, Je binti huyu ana ujasiri gani mpaka kusema chochote? Au anataka kunishikisha
rushwa au labda ana mapepo ya ngono ya kikabila?????????????

Nikapata wazo na kumwambia kuwa sawa nitampa usahili siku ya pili aufanye ila kabla ya siku ya pili ningependa kulala naye pia.

Binti akakubali na kumwita dereva ampeleke hotelini kwa ahadi kuwa nitamfuata yule binti mida ya usiku ili nijilie vyangu.

Usiku ule nikawahi kwenda pale na akanikuta nakula huku yeye akitoka chumbani na kuniambia kuwa alikuwa akinisubiri na kisha
tukajumuika chakula baada ya kumdanganya kuwa nilibanwa na kazi.

Baada ya chakula nikamkimbia na siku ya pili alionyesha kutopenda ingawa mimi nikajikausha
kama sielewi na baada ya usaili ule akabahatika kupata kazi kwani wenzangu walimpenda pia.

Ikapita miezi na utendaji wake ukiwa wa kutukuka na hatimaye akaonyesha kuwafurahisha wengi nami nikapitia mwanya huo
kumuuliza ni kwanini aliamua kuniambia angenipa chochote hata mapenzi kama ningempa kazi na anajisikiaje nikiwa sijamuomba
anipe mapenzi na kumkimbia?

Alinijibu majibu yaliyonifanya niishiwe nguvu kwani alisema,

" Miaka miwili iliyopita baba, mama, kaka, mdogo wangu na dada yangu walipata ajali
wakitoka katika mahafali ya dada yangu katika chuo fulani ambako dada alikuwa akihitimu na
kufa wote.

Nimenyang'anywa kila kitu na ndugu wa baba na nimekuwa natafuta kazi bila kupata na kila
mtu akinitaka nilale nae ndio anipe kazi bila mafanikio, hivyo nikaona nikufanye ulale nami ili nipate kazi na pesa ya kujisitiri"

Baada ya kuongea hayo aliniacha nikilia na kuamini kuwa kuna watu huchukua maamuzi magumu kutokana na matatizo yanayowakumba.

Kuanzia sasa nahakikisha nakuwa mfano wa kuigwa kuwasaidia wenye shinda bila kutegemea
malipo na wewe je?

Share na comment kama umeumia na umejifunza kitu

like Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: