Nilimshuhudia mke wangu akimegwa kisela mbele yangu kisa nilijifanya kipofu.......... Uzalendo ukanishinda

21:06:00 Unknown 0 Comments

Nilisimamishwa kazi kutokana na baadhi ya vitu kuibiwa katika store ya kampuni na mimi wakati huo nilikuwa ndio msimamizi mkuu wa store katika kampuni hiyo ya ujenzi.

Wakati huo nilikuwa nimebahatika kujenga na kuwa na gari langu la kutembelea lakini vyote hivyo vilitakiwa kuchukuliwa na kampuni kwani fedha ambazo nilitakiwa kuzilipa kama fidia ya vifaa vilivyoibiwa ilikuwa ni kubwa sana.

Huwezi amini maisha yakaanza kuwa sio ya kawaida kwangu na mke wangu akawa hana raha kabisa na kwa kuwa sikuwahi kutaka kufikiri kama mkwe wangu hata kama hatukubahatika mtoto aumie kwa maisha ya shida nikaona ni bora nisafiri na kwenda jijini dar nikitokea mbeya.

Dar ni mji wa pilika hivyo nikajikuta nikiomba kazi na kupata katika hoteli moja kubwa pale na kuanza kuitumikia nafasi hiyo mpya maishani ya kuwa mfanya usafi na mara moja moja nikisaidia jikoni au kuhudumia wateja kama mtu angechelwe kufika.

Ilinibidi nifanye hivyo kwani kila mwisho wa mwezi nilitakiwa kutuma kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya matumizi ya mke wangu kwani tulikubaliana kuwa nitafanya kazi kwa miezi michache na kutafuta pia mtaji wa kwenda mbeya kuanza biashara zetu.

Nilifanikiwa kuchukua mkopo mdogo pale ofisini na kumtumia mke wangu ili afungue ofisi yake (salon) kama alivyoomba ili aweze nae kusaidia kuongeza kipato jambo ambalo kwangu lilikuwa ni zuri sana kwangu.

Kutokana na ule mkopo maisha yangu yakawa ya shida zaidi pale dar na kama haitoshi ikawa kila mwezi mimi naomba salary advance na maisha yakasonga kwa taabu sana.

Miezi kama nane baadae nikawa sasa nimefikia kiwango cha kukosa hata nauli na ofisi imekataa kabisa kunipa salary advance ili nijikimu na kupata nauli zaidi wakaniambia nije na kuanza kukaa pale pale hotelini jambo ambalo nilitambua wazi kuwa hawakutaka kusema wazi kuwa sasa nitakuwa mlinzi ila ndio ukweli.

Hali ikazidi kuwa ngumu na mbaya zaidi hata kazi nje ya hotel zikawa ngumu nikaanza kukata tamaa na mke anadai hana kitu. Kuna mteja mmoja alikuwa ananipenda sana pale hotelini na alikuwa akija mara kwa mara ikanibidi nimvizie siku hiyo nakiwa anatoka chumbani kwake kwenda kazini na kumwambia shida yangu ingawa akaonesha hana kitu.

Zikapita kama siku nne na kuna siku usiku wa manane nikiwa nimekaa kakaa pale hotelini nikashtushwa na sauti za watu wakibishana na nikashuka chini kuchungulia dirishani mlinzi alikuwa kalala na yule mteja kazingirwa na watu akiwa anashuka kwenye gari lake ili afungue geti baada ya kupiga honi bila mlinzi kufungua.

Nilishuka haraka kwa tahadhari na kuchukua mawe kadhaa na kuawarushia wale jamaaa na kwa kuwa hawakujua nilikuwa upande gani kwa hofu wakaanza kuondoka na kukimbia na kumwacha yule jamaa akiwa kaanguka chini na kaukumbatia mkoba wake.

Alinishukuru na kisha akaingia chumbani na siku nne baadae iliitwa ofisini na meneja wangu kuwa kuna mtu alihitaji kuongea na mimi mbele ya meneja. 

Alikuwa ni yule mteja wetu na kuniambia kuwa siku ile kama nisingemsaidia pale alikuwa na madini na wale majambazi wangemdhuru na kukimbia na mali hizo ambazo ni mamilioni ya pesa.

Baada ya kuongea hayo alinikabidhi cheki ambayo kamwe sitaka niisahau kwani ilikuwa na shilingi milioni 30. Sikuona umuhimu wala ulazima wa wewe kunipa kiasi hicho chote ila nikamshukuru Mungu na kuamini Mungu hujibu sala zetu kwa muda muafaka.

Niliomba kuacha kazi pale ili nirudi Mbeya na kitu cha kwanza nilitaka hata nitumie milioni saba tu kumpa zawadi mke wangu ya gari ambalo litatusaidia pale nyumbani na nyingine niziwekeze kwenye biashara ili sasa tuweze kuwa na kipato cha uhakika.

Nikiwa bado sijamwambia mke wangu kuhusu bahati hii ili kumfanyia surprise mara dada yangu alinipigia simu kuwa hivi sasa mke wangu yeye akawa na mahusiani pale mtaani na karibia vijana wote.

Nilishikwa na mshangao na hata kabla sijawa ni jibu sahihi na rafiki yangu mmoja wa kike pamoja na kaka yangu mmoja pale mtaani wakanipigia na kuniambia habari ile ile. Mwanzoni nilifikiri labda ni kwa sababu ya ile salon ndio maana wanampiga vita lakini sasa nikaona kuna ukweli.

Niliamua kumpigia mke wangu na kumwambia kuwa nitarudi ila naumwa na hivyo sitaweza kuendelea na kazi,  nikurudi nyumbani na nilipofika mbeya nikapokelewa ingawa mke wangu alikuwa kabadilika sana.

Niliporudi yangu siku ya kwanza ananipokea nilimwambia juu ya mimi kupatwa na ungonjwa ulionisababishia macho yangu kupatwa na upofu na kuwa siwezi tena kuona zaidi ya kukaa pale nyumbani na wakati huu nikiwa kama mtoto ninayehitaji msaada wake kwangu kuanzia kuniongeoza, kuvaa na mengineyo.

Kiukweli nilioa akipatwa na taabu sana kuupokea uamuzi huo na hata wakati mwingine kunifanyia vitendo vya kejeli mbele yangu akijua mimi sioni lolote lililokuwa likiendelea.

Alifikia pabaya kiasi cha kuingia na wanaume ndani akijua mimi sioni nilijikaza kisabuni nikitaka nione mwisho wake utafikia wapi nna wakati huo akawa hataki kabisa kulala na mimi akidai hayuko tayari kwa mtoto na mie nikaona sisiwe taabu nikasingizia kuwa ugonjwa umenifanya nisiwe na hamu ya tendo la ndoa.

Sikuwa na pupa maana hata nilipojaribu kuongea na baadhi ya marafiki na ndugu zake walidai namwonea mtoto wao hivyo nikaona nisubiri mwisho wa mchezo nione yepi yatajiri. Kuna rafiki yangu mmoja aitwaye Fred yeye nilimpa fedha kiasi na kumwomba awe anakuja kila weekend kunipa hiyo hela kidogo kidogo kwa ajili ya matumizi.

Mbaya zaidi kila aliponiletea hizo hela mke wangu alizichukua na kwenda kula maisha na vijana wake na muda mwingi niliacha akijua sielewi lolote. Nikapanga mpango wa siri bila yeye kujua na kumfanya agombane na wale vijana na hali ilipozidi kuwa ngumu nikaandaa sherehe ya siri ya siku yake ya kuzaliwa,

Ilipokaribia siku hiyo nilialika marafiki zake wote waliokuwa wakimtetea na baadhi ya ndugu zake na siku ya sikukuu watu baada ya kufurahi nikaona niwape surprise ya kuwaambia muda wote huo sikuwa mgonjwa wa macho wala nini na kama haitoshi nilikuwa nikimrekodi kila alichokuwa akikifanya na wale wanaume wake pale kwangu akijua sioni na kisha nikawapa na mkasa wangu ule wa dar es salaam.

Ni mwezi wa nne sasa tangu apone kichaa na sasa karudishwa kijijini na mimi sasa nimeanza maisha mapya ya kuwa peke yangu huku nikijiuliza ilikuwaje abadilike kwa muda mfupi vile au mwanzoni alinipenda kwa ajili ya fedha?

Ama kweli kama huna hela hata mapenzi ya dhati utaishia kusimuliwa



 

You Might Also Like

0 comments: