Wanaojua mambo daima huonesha kwa vitendo na sio kwa kelele..

11:57:00 Unknown 0 Comments

Kwa kawaida sisi tuliobahatika kufyatua matofali tumefanikiwa kujifunza kitu kimoja cha muhimu sana.
Unapobeba debe tupu kwenda kuchota maji basi hupiga kelele sana ila unaporudi ukiwa na maji basi debe huwa kimya sana tofauti na awali.

Hapa najifunza pia hata katika maisha ya kawaida watu wenye uwezo wa mambo fulani, wanajiwezam kiuchumi watu wenye vichwa vyenye madini au ndimi zenye kutoa matamko yenye maana kubwa huwa hawapigi kelele zaidi ya kuwa kimya na vitendo vikiongea zaidi.

Ni bora kuwa mwelewa wa mambo mengi na ukatufahamisha hilo kwa vitendo na sio kupiga kelele.
Maisha yetu yanataka watu wenye vitendo kuliko kelele

Mpaka sasa sijui naandika nini ila kama wewe umeelewa basi nikutakie siku njema

You Might Also Like

0 comments: