Mambo 30 muhimu ya kufanya ukijikuta uko katika msongo wa mawazo usiotibika
1. Jaribu kufanya kitu amabcho umekuwa ukifurahia kila ufanyapo:
Unapokuwa na huzuni unatakiwa kuwa kufanya vitu vitakavyokupa furaha.. na katika kila hali hata kama inaumiza kiasi gani lazima uamini mambo hutokea na kwasababu na silaha nzuri zaidi ni kujipa furaha ili uweze kuimudu hali.
2. Jifunze vitu vipya:
Tunajifunza kila siku tena vitu vipya.Kujifunza vitu vipya vitakufanya kuwa busy na kujikuta ukiishinda hali yoyote inayosababishwa na msongo wa mawazo.
3. Jipe zawadi kwa kuwa na hali nzuri ili usahau yaliyopita:
Tabia nzuri itaongea na wewe na kukupa nguvu.Jipe pongezi kwa kila hatua utakayoivuka kwa ushindi.
4. Kuwa na furaha pale utakapokula chakula ukipendacho:
Kila mtu ana chaguo la chakula akipendacho. unapokuwa na huzuni au mawazo ukajikuta unapata kitu ukipendacho basi hata kumbukumbu za vitu vizuri hukujia na kusahau yaliyopita.
5. Chukua hatua kuelekea malengo yako:
Unapokumbuka malengo yako unakuwa umejipa nafasi ya kuanza kuiona baadae yako kwa namana nzuri.,jitahidi kujituma na kufanya kama malengo nyako hiyo itakupa nafasi nzuri ya kufanikiwa na kusahau yaliyopita.
6. Kepnda mifugo yako au vitu vikuzungukavyo
Kama una mifugo mfano kuku, ng'ombe au mbwa jaribu kupata muwa wa kuwahudumia ukijaribu kuwa nao karibu kwa muda huweza kukupa furaha na kusau yanayokusibu
7. Punguza hofu:
Utakapoanza kujifunza kutokuwa na hofu ndio utagundua njia mpya za kukupa nguvu na kukupa maisha yenye furaha zaidi..
8. Nini ukipendacho zaidi?
Kwa mfano mimi FULEDI napenda sana kusoma vichekesho , kungalia filamu za vichekesho na kuandika vichekesho huku nikisoma comments kutoka kwa marafiki baadhi ya nyakati kama njia ya kujipa furaha.
Na wewe unaweza kuwa na njia mfano kuimba au hata kusikiliza nyimbo jaribu kuvipenda zaidi ya huzuni itakutoweka.
9. Marafiki wa kweli:
Kuwa na marafiki wakweli inasaidia sana hivyo tumia muda wako kuwa na marafiki wa kazribu sana na jaribu kubadilishan a nao mawazo na kufurahi nao.
10. Tabasamu:
Tabasamu ni dawa nzuri sana ya kuondoa msongo wa mawazo katika maisha. Tabasamu kila wakati na ukiwa tayari kwa lolote na utashinda.
11. Jipe changamoto
Jaribu kujiambia kuwa wewe ni jasiri na kuwa ni jasiri zaidi katika kipindi hiki tofauti na mwanzo.
12. Tumia muda wako kuwa na watu wanaoku-inspre au kusoma vitu vinavyokupa mwanga mpya kutoka kwa watu wa aina hiyo
13. Jaribu kila mara kutafuta furaha hata katika mambo madogo.
14. Share mawazo yako kwa watu uwapendao na kumaanisha
15. Soma habari zitakazokupa furaha mpya.
16. Kufanya mambo mema yatakupa furaha hivyo fanya mambo mema wakati wote.
17. Uwe makini, mwelewa na mwajibikaji
18. Jaribu kufanya ambo mapya kwa umakini
19. Jaribu kuicheza michezo uipendayo hukusaidia kuyasahau yaliyopita
20 Kuwa mtu wa tahadhari na amini katika mabadiliko
21. Heshimu maamuzi ya wenzio, furahia mafanikio yao nawe chukua changamoto
22. Jipe moyo wa kuanza maisha mapya ukijijengea furaha
23. Jipe hongera katika kila hatua
24. Fikiria juu zaidi
25. Samehe, sahau na zaidi jisamehe na wewe
26. Uwe mtu wa kutoa na washangaze wenzio kwa zawadi za mshangao jambo hili laweza kukupa furaha kwa jinsi watu watakapolipokea.
27. Uwe huru kwa mazingira yako
28. weka mipango mizuri ya kuja kufanyika kwa baadae
29. badili ratiba yako na kuifanya iendane na sasa
30 kuwa karibu na familia yako na tunza kumbukumbu
0 comments: