MTU mmoja alifariki na kwenda jehanamu. Kufika huko akakuta kuna jehanamu tofauti tofauti kwa kila nchi

16:49:00 Unknown 0 Comments

MTU mmoja alifariki na kwenda jehanamu.
Kufika huko akakuta kuna jehanamu
tofauti tofauti kwa kila nchi. Akaamua
kuzunguka zunguka ili aweze kuipata
jehanamu yenye maumivu kidogo zaidi.
Akaiendea jehanamu ya Ujerumani. Akamwuliza
mtu aliyemkuta mlangoni.
"Wanakufanyaje ukiingia humu?"
Akajibiwa. "Kwanza wanakuweka kwenye kiti cha
umeme kwa saa moja, kisha
wanakulaza kwenye kitanda cha mizumari kwa
saa moja nyingine. Kisha anakuja
shetani wa Kijerumani anakucharaza bakora
kutwa nzima."
Mtu huyo hakuipenda kabisa jehanamu hiyo.
Akaamua kujaribu jehanamu za
Marekani, Uingereza, Urusi na nyinginezo nyingi.
Lakini akagundua kuwa zote zina
adhabu sawa tu na jehanamu ya Ujerumani.
Kisha akaifikia jehanamu ya Tanzania.
Akastaajabu kuona kuna foleni ndefu kweli
ya watu wakisubiri kuingia humo. Kwa mshangao
usiosemekana akauliza, "Jamani
kwani humu wanawafanyaje?"
Akajibiwa, "Kwanza wanakuweka kwenye kiti cha
umeme kwa saa moja, kisha
wanakulaza kwenye kitanda cha mizumari kwa
saa moja nyingine. Kisha anakuja
shetani wa Kitanzania anakucharaza bakora
kutwa nzima."
Akazidi kustaajabu. Akauliza, "Lakini mbona
kinachofanyika humu ni sawa kabisa
na kinachofanyika kwenye jehanamu zingine,
sasa kwa nini hapa kuna foleni
kubwa sana watu wote wanakimbilia huku?"
Jamaa mmoja akamshika mkono. Akamvutia
pembeni. Akamnong'oneza, "Watu
wanakimbilia huku kwa kuwa jehanamu ya
Tanzania haina umeme wa uhakika,
unakatika katika kila dakika kwa hiyo kiti cha
umeme hakifanyi kazi. Halafu pia
misumari ilishalipiwa lakini wala haijaletwa na
mzabuni kwa hiyo kitanda cha
humu ni raha tu kukilalia. Na jambo jingine ni
kuwa shetani wa Kitanzania
alipokuwa duniani alikuwa mtumishi wa umma.
Kwa hiyo ameshazowea kufika
ofisini na kusaini kitabu cha mahudhurio na
kisha kuondoka zake kwenda kufanya
shughuli zake binafsi."


UWAPO MBEYA TEMBELEA WWW.KARIBUMBEYA.COM.....TANGAZA BIASHARA YAKO BURE HAPA
Photo: UWAPO MBEYA TEMBELEA WWW.KARIBUMBEYA.COM.....TANGAZA BIASHARA YAKO BURE HAPA
47 people reached

You Might Also Like

0 comments: