Ukisikia zali la mentali basi wewe msome huu jamaa
Jumapili moja mika 20 iliyopita kijana mmoja alihudhuria ibada ya jumapili kama kawaida yake.
Kanisani walihubiriwa juu ya kuwa mwaminifu katika jambo dogo kwani ni katika hayo mambo madogo utajipatia mambo makubwa.
Baada ya ibada kijana akiwa anarudi alikutana na bibi mmoja mzee ambaye alikuwa kaumizwa vibaya na gari lake likiwa limeibiwa.
Kijana alifanikiwa kumnyanyua yule bibi pale alipokuwa amekaa na kugundua alikuwa na hela nyingi kazilalia pamoja na baadhi ya vitu vyake vya thamani.
Alivikusanya vile vitu na kuvihifadhi na kisha akaomba msaada wa gari na kumpeleka yule bibi ambaye alipoteza fahamu hospitali.
Kijana alimtembelea yule bibi kila suku mpaka akapona na siku bibi anaruhusiwa akamshukuru sana yule kijana kwa moyo wake ingawa aliumia kwa kuwa aliibiwa gari na kila kitu hasa baadhi ya mikufu na vito vya thamani alivyopewa zawadi na marehemu mme wake pamoja na fedha.
Pamoja na kijana kuwa na maisha magumu lakini alimpatia vile vitu vyote alivyoviokota siku ile. Bibi alifurahi sana na kumshukuru sana yule kijana.
Kama ilivyomatarajio ya watu wengi kila mtu alifikiri kijana yule angepewa fedha nyingi lakini bibi alimpa ufunguo kijana yule na kusema autunze.
Ilipita miaka mingi siku moja kijana akasoma kwenye gazeti kuwa bibi mmoja tajiri sana alifariki na kuacha wosia kuwa kila mjukuu wake aliachiwa kitu cha urithi hivyo kama mtu uliwahi kupewa kitu na bibi huyo uwasiliane na familia.
Kijana alifanikiwa kuwasiliana nao na alipofika katika mji ule kumbe ile funguo ilikuwa ni ya jengo moja kubwa ambalo bibi huyo alikuwa akilijenga kabla ya kuvamiwa na ndio ikawa zawadi yake.
“Mtu aliye mwaminifu katika lililo
dogo zaidi ni mwaminifu katika lililo kubwa pia.”— LUKA 16:10 .
dogo zaidi ni mwaminifu katika lililo kubwa pia.”— LUKA 16:10 .
Rafiki
Nakuombea nawe uwe mwaminifu katika jambo dogo kwani ndio baraka na mafanikio yako yalipo
Comment AMEN na kushare ujumbe huu kama njia ya kuufanya ujumbe huu uwe wako ukikukumbusha uwepo wa Mungu maishani mwako
Karibu Mbeya shared a link.
NAFASI ZA MASOMO – MARCH INTAKE 2015
0 comments: