Binti aliyewaliza wengi baada ya kifo chake............. Inaumiza sana
Baada ya mahusiano ya zaidi ya miaka mitatu na siku kadhaa kijana alishindwa kuhimili shinikizo la ndugu na kumwacha mpenzi wake kwa madai kuwa sio wa hadhi yake.
Akapewa mke mpya na baadae kuanza maisha mpya na ndugu wakifurahia uamuzi wao wa kumpa kijana wao mke mpya huku wakimsahau yule dada wa kwanza.
Binti yule wa kwanza akaondoka na kwenda mji mwingine kuanza maisha yake huku akijikita katika biashara zake.
Siku zikapita na kila mtu akasahau mkasa ule wa binti aliyefukuzwa kabla ya kijana kuanza kuumwa.
Wakazunguka kila hospitali bila kupata tiba mpaka pale walipokuja kugundua kuwa figo zake zimeharibika na hawezi tena kupona kama sio kupata figo kutoka kwa mtu wa karibu au afe.
Ndugu na marafiki wakamkwepa na kumwacha akiwa kalala pale hospital bila ya msaada na kila mmoja akiogopa kutoa figo kumpa kijana apone na mbaya zaidi hata mke wake mpya akawa amekimbia na kurudi kwao.
Mama wa kijana alizidi kumtunza kijana akiwa hana namna ya kumsaidia kwani kwa uzee ule alikataliwa kutoa figo yake imsaidie mwanae apone.
Siku zikasogea na yule mchumba wa kwanza aliyefukuzwa akapata habari za mpenzi wake wa mwanzo kuwa hali sio nzuri. Kwa huruma akaja mpaka hospitalini na kukubali afanyiwe upasuji na atolewe figo moja.
Kabla ya upasuaji aliomba karatasi na kuandika kitu na kumpa daktari amwekee. Kwa bahati mbaya baada ya upasuaji yule dada alifariki na kijana baada ya wiki kadhaa alipona na kuwa mzima kabisa.
Siku moja akaenda hospitali ili amshukuru daktari na wote waliomsaidia akiwa pale hospitali, akiwa chumbani kwa daktari alipokea karatasi kutoka kwa dakatari na kuambiwa kuna mtu aliyemsaidia kutoa figo kabla hajafa alimwachia karatasi... Kaka kabla ya kusoma akaumia sana na kusema laiti mtu huyo angekuwa mzima amshukuru kwa moyo ule wa huruma na kisha akaifungua ile karatasi na iliandikwa:-
"Mpenzi wangu Nolesy kama unausoma ujumbe huu basi ujue wewe ni mzima na umepona sasa baada ya mimi kukupa figo yangu.
Nilikupa moyo wangu ukauumiza sana na kunipa majeraha makali huku ukinitazama bila huruma.
Sasa nimekupa figo yangu, naomba uipende sana hata kama hautaniona mimi kama ilivyokuwa kwa moyo wangu.
Nakutakia maisha mema.
Zilipendwa wako Habiba"
Siku moja baada ya kuusoma ule ujumbe kijana yule siku ya tatu yake alikutwa amekufa kwa kujinyonga.
Rafiki shikilia ulichonacho sasa kwa maana ni baraka kwako na huwezi ona umuhimu wake mpaka utakapokipoteza au kukikosa kabisa
Siku njema
Kama umeipenda ruksa kushare
0 comments: