Binti aumbuka akitafuta mchumba mtandaoni

09:21:00 Unknown 0 Comments

Dada mmoja alimpata mchumba mwenye asili ya kiarabu kwa njia ya facebook.
Baada ya kudeti nae kwa muda mrefu aliamua kumwambia mama yake kuwa amempata mpenzi wake na anataka kuja kuleta barua ya posa yenye fedha za kitanzania milioni tano ndani yake.
Mama alimuuliza, "Je umewahi onana na mtu huyo?"
Binti akamjibu mama yake kuwa hapana sijawahi onana nae ila nawasiliana sana kupitia facebook.
Mama alilia sana pamoja na kuwa yeye ni maskini ila aliomba Mungu ampe mwanae ulinzi wa kutosha na busara katika maamuzi na ikiwa sio mapenzi yake atengue uchumba huo kwani alidhani mwanae atapatwa na madhara makubwa kwa kuolewa na mtu asiyemfahamu.
Wiki moja baadae dada yule akaunti yake ya facebook ilivamiwa na wezi wa mtandao na kuibadilisha pasiwedi yake na dada kushindwa kuingia tena na kupotezana na mpenzi aliyekusudia kuleta barua ya posa.
Siku moja dada yule alirudi nyumbani akiwa analia baada ya kuona taarifa ya habari ikionyesha yule bwana katiwa mbaroni kwa kuhusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Mama yule baada ya kuambiwa na binti yake kuhusu mme huyo alipiga magoti na kumshukuru Mungu akisema, "Eeh Mungu, nashukuru kwa kuwa umeyajibu maombi yangu kwa kufichua uozo wa mkwe niliyetaka kuletewa na binti yangu, na umemwokoa mwangu katika mikono ya adui shetani.....Lihimidiwe jina lako takatifu AMEN"
Nami nakuombea rafiki wa fuledi katika mwaka 2014 kila jambo baya ambalo mwovu shetani na vibaraka wake wanataka kukuletea katika kazi yako, afya yako, familia yako na maeneo mengine yashindwe kwa nguvu za Mungu.
Comment neno "Haleluya" kisha share kama unaamini uweza wa Mungu katika kuifanikisha mipango yako mwaka 2015

You Might Also Like

0 comments: