" Daima mwanamke kwanza"
" Daima mwanamke kwanza"
Aiseee hii sentensi nakubaliana nayo kwa asilimia zote, sio tuu kwa sababu mtoto wangu wa kwanza ni ni wa kike kuwa najitahidi kuanza sasa kuona umuhimu wa mwanamke kwa kuwa nitapenda kuona anapewa kipaumbele.. HAPANA
Nasema hivyo kwa kuwa nafahamu fika nafasi ya mwanamke yoyote katika jamii yetu. Achana na yale ya kutulea ambayo wengi wetu huona kama ndio uanamke kama ilivyo kwa mwanamme kuhakikisha anatoa jasho ili familia iwe na kipato ila mwanamke anacheza nafasi kubwa mmno.
Kuna wakati nilishawahi kuwa na mchepuko mmoja na nikajifanya nikoleze mapenzi kwa kujitahidi angalau weekend niwe nawahi kuamka namtayarishia ka breakfast anapoamka aone pale chumbani kuna kitu kinamsubiri. Siku ya jumapili mchana nipike tule na nimwandalie kavazi tutoke out.
Amini usiamini niliweza kwa wiki mbili tuuu nikajikuta nimechoka ... lakini leo najiuliza wao wanawezaje tena sio kwa wiki mbili yaani tangu unamuoa au unakaa nae kinyemelea mpaka kifo kiwatenganishe kama sio talaka.
Kwa hilo huwa nawaheshimu na kinachonifanya ni waheshimu tena zaidi ni pale ambapo pamoja na majukumu hayo yote bado mzee utataka msaada kitonga kila usiku bila kufikiri huyu mtu kachokaje ila yeye ataoesha poa tuu... hapa wananishangaza maana hata laptop yangu huwa inastaki ikipata mzigo hevi sasa wao sijui huwa wanawezaje kuyakabili majukumu hayo yote.
Ila kuna baaadhi nafikiri hii hii senstensi ya "mwanamke kwanza" wao wanaichukulia tofauti. Kwani mimi nafikiri maana yake ilikuwa ni kumpa mwanamke nafasi ya kuwa mbele kwa kila jambo jema tukiamini kwa kuwa mstari wa mbele ni rahisi sana kwa yeye kuibadilisha jamiii.
Mwanamke ana uwezo mkubwa sana wa kuleta mabadiliko hasa akipewa hiyo nafasi ya mwanamke kwanza..... ila sasa naandika huku nikiwa nimenuna baada ya kumpata mchepuko huyu mpya ambaye mwanamke kwanza kwake ina maana tofauti.
Yeye mwanamke kwanza iko kwenye vibomu, mkiwa out ahudumie wa kwanza ila kwenye bili mwanamke mwisho. Kila hitaji la starehe akitoa aidia basi inatakiwa usiangalie nyuma kwa kuwa mwanamke kwanza.
Naona nikiendelea kuchepuka nae lazima atachapwa ngumi tuuuu maana mizinga inayoshikiliwa na falsafa ya mwanamke kwanza imezidi na hakuna namna zaidi ya kuchapwa tuu


0 comments: