Kisa cha binti wa facebook aliyenunua gari kwa mkopo wa Saccos

15:33:00 Unknown 0 Comments



Ukitaka kumjua Msichana aliyenunua gari kwa Mkopo wa Benki au Saccos au kuhongwa gari baada ya kufunua kombe wala usipate shida,we mfuatilie Aina ya Status atakazoandika tu utajua anakutumia salamu kwamba NA MIMI NINA GARI SASA HIVI Indirectly....Utasikia tu
"AC yangu ina vumbi sana jamani nani anajua fundi mzuri pls help"
Oh My Ghosh,yaani masaa 2 sijasogea hata mita 10 this Kimara Jam sucks"
"Jua kali sana leo Dar guys hadi AC siisikii kabisa.Na nyie mmeona guys au ni mimi tu?"
"What a bad day,gari haiwaki SHIT"
"Honi yangu leo haipigi kabisa sijui imeingia mende jamani please help"
Yaani atajisemesha weee kwa topic isiyo hata na ulazima,sasa kama mende wameingia kwenye Honi ya gari lako ukiposti FB sisi ndo tunauza dawa za Mende kwenye Wall ama??
Wajuzi wa mambo ndo tunakutambua kwamba unatupa taarifa kwamba hatutakiona tena kikwapa chako cha njano kwenye daladala
HAWAWEZAGI KUJIFICHA KABISA HAWA WENZETU..

You Might Also Like

0 comments: