Mambo 7 muhimu ya kuyafikiria Kabla ya kuamua kuoa au kuolewa

10:45:00 Unknown 0 Comments



Unahitaji kuwa katika ndoa yenye furaha na utimulifu? Ni rahisi  sana ingawa pia unatakiwa kuwa na mkusanyiko wa baadhi ya mambo yenye uhalisia kutoka kwako kwanza.

 Haya ni baadji ya mambo ambayo watakiwa kutamka kwa kinywa chako kuwa unayaweza kabla ya kuelekea barabara ya NDOA.........

Je wewe ni mcheshi?

Kuwa mcheshi ni jambo la muhimu sana na mtu wa kwanza ambaye unatakiwa kuwa mcheshi au na furaha kwake ni wewe mwenyewe.

Unatakiwa kuwa na uchangamfu na ucheshi katika maisha na kutengeneza mazingira ya kufanya kila kitu pembeni yake kifurahie uwepo wako hasa kwa wanaokuzunguka na wa muhimu pia ni huyo ambaye unategemea kuwa nae. 

Unatambua kuwa utatakiwa kujibiidisha?

Watu wengi wanaamini ukishaoa au kuolewa basi kazi imeisha kwani ndoa itaenda yenyewe. Ndio ni kweli kwa masaa au siku inaweza ikaenda yenyewe lakini kumbuka kuna miezi na miaka ijayo ambayo mtatakiwa kuendelea kushi hivyo utatakiwa kujibiidisha kuipa ndoa yako afya na kuwa yenye furaha, amani na maendeleo.

Hivyo hapo kuna kazi ya ziada ambayo inahitaji team work ya watu wawili lakini idadi kubwa ya watu huamini ni kazi ya mmoja au hata kusukumizia majukumu kwa mmoja wao.

Unatambua kuwa ndoa sio nusu kwa nusu ?

Sasa tulipoongelea team work kuwa mtashirikiana maana yake sio kila mmoja atatoa nusu ya nguvu zake, na kama ulifikiria hivyo basi acha kwanza kufikiria kuolewa au kuoa.

Kunasiku utatakiwa kujitoa kwa zaidi ya asilimia 95 bila ya kujiuliza kwa nini mwenzako hajatoa iliyobaki pia, maisha ya ndoa yanataka kujitoa bila kuangalia mwenzako kafanya nini au kuweka katika kumbukumbu na kuja kulalamika.

Kwa kufanya hivyo unatoa nafasi kwa upande wa pili nao kujitoa zaidi na hapo ndoa inakuwa na afya, ingawa wengi bado wanaamini nusu kwa nusu.

Je wewe ni mwepesi wa kukubali madhaifu ya wenzako?

Ameoga akatupa taulo chini, umedeki akaindia na viatu, mezani wakati wa chakula sio mstaarabu, anakunywa pombe na wewe  hautumii, anavuta sigara..............

Huwa inakuwa ni ngumu sana kwa wengi kuendelea kuvumilia hata kama hapo awali mtu aliona kuwa ni kawaida. Jambo la msingi hapa ni kuendelea kuyapokea mabaya na mazuri yake na kujaribu kutafuta njia isiyo na madhara ya kukabiliana hata kuyarekebisha machache  ingawa huchukua muda.

Je unamatarajio katika ndoa yako ambayo yapo kichwani au penginde ndio msukumo wa wewe kuolewa au kuoa?

Kama swali hili ulisema NDIO na uko kwenye mahusiano hebu anza mchakato wa talaka.

Kuwa na matarajio ya msingi kama vile mwenza kuwa mwaminifu, ndoa kuwa na furaha wakati wote, kuishi maisha ya furaha bila kuwa na nyakati za huzuni, mwenza kuwa mkweli na yote haya kuwa kifurushi kilichoambatana na nia ya wewe kuingia kwenye ndoa , basi ndugu wewe rudi tuu kwa babu pale iyunga uendelee kulima maharage kwani ndoa kwako itakuwa mzigo.

Wengi hapa wanaathiriwa na filamu za bongo movie au wale wanaojiita motivational speakers ambao wataiongelea ndoa kwa mazuri tuu na kukufanya uamini kuwa, ndoa ni kama simulizi nzuri ya mapenzi tena ya kihindi ambayo daima itakuwa na mapito mazuri, nyimbo za mahaba kwa mbali na mwishowe wapendano wanaishia kuendelea kuishi kwa furaha.

Ndoa ina miskukosuko, majanga na mazuri mengi pia ambayo wawili mnatakiwa kuishi kwa kujifunza na kujinoa kupitia hayo bila ya kukata tamaa na kutatua kila jambo kwa ushirikiano na sio kwa kushirikisha.. hivyo unatakiwa kujiandaa kwa sura zote mbili

Je, unajua kulinganisha ni hukumu ya kifo kwa ndoa ?

Kama ilivyo kwa alama za vidole vyetu (fingerprints),Ndoa zina utafauti kati ya ndoa ya yule, au ya mimi fuledi na ya kwako wewe utakayokuwa nayo, kwa sababu ndio ni muunganiko ya wawili ambayo na wana tofauti zao na sasa wamekuwa kitu kimoja.

 Badala ya kumpigia kelele mmeo kuhusu kuwa na out za kimahaba kwenda chakula cha jioni katika hoteli fulani, kusafiri na kwenda nje ya miji kwa likizo tamu za kimapenzi kama marafiki zako na waume zao, wewe TABASAMU.

Huwezi jua wenzako wakiwa katika chakula cha jioni huko out na wapenzi wao ni mara ngapi watalia baada ya kuambiwa maneno ya kuumiza na wapenzi wao, mara ngapi watalala vyumba tofauti au vitanda tofauti baada ya kugombana kwani mme alionekana akiwa na binti mwingine pale beach au meseji iliingia na mambo mengine mengi.

Kumbuka hutaweza kujua nini kinaendelea ndani ya milango ya vyumba vyao iliyofungwa hivyo wewe jaribu kukaa na mmeo na kmabadilishana mawazo yanayoweza kuwapa furaha na maendeleo yenu.

Kama mme hajanunua mark x usimfanye akope au harusi yako iwe ya kunga mwaka na mweza mmoja baadae hamna kodi ya nyumba... Ila mark x taaamu bwana....ha ha ha ha

Je unajua mpenzi wako ana lugha mbili?

Nimekuwa nikisoma simulizi post za kinadada wewengi pamoja na baadhi ya wanaume pia hapa facebook, nimesoma simulizi nyingi kuanzia kina sindi ya Laura Pettie​, salma ya Kalmas Konzo​ na huba ya fadhy mtanga na nyinginezo nyingi.

Ukisoma utagundua vilio vya mabinti au maumivu ya mapenzi yanatufanya watu tufikiri labda wanaume wanatokea sayari ya Mars, na wanawake wanatokea sayari Venus. Kwamba bado ni ngumu kwa jinsia hizi mbili kuelewana.

Mme anaweza asikuambie  “I love you” mara 20 kwa siku ila akakumbuka kukuwekea mafuta au credit kwenye simu yako.Anaweza asikutoe out siku yan kumbukumbu yako ya kuzaliwa ila jumamosi moja akakupeleka shopping au akakaa na wewe na kukusaidia kupika.

Cha mshingi ni kukumbuka kujifunza kushukuru na kuelewa kila atakachojitahidi kukufanyia na kuonesha umefurahia...... 

Ndo yenye mafanikio inatumia gharama kubwa sana... sio ya hela tuu ila kufanya hivyo hapo juu hata mimi naendelea kujifunza 

Soma namna ya kumfanya binti akupende daima kwa kubofya  HAPA

You Might Also Like

0 comments: