Njia rahisi ya kumpiga mkwara boss wako jumatatu hii
Jamaa alikosea ofisini kupiga simu na kumpigia simu bosi wake kwa bahati mbaya akiwa na dhumuni la kumpigia mfanyakazi mwenzake ili amzingue....Jamaa: "Oya we mpuuzi lete chai vikombe viwili haraka mezani kwangu na chapati 3..!!!"
Bosi: "Hivi unajua unaongea na nani??!"
Jamaa: Acha upuuzi dogo fanya kama ulivyoambiwa lete chai fasta
Bosi: eti Hivi unajua unaongea na nani??!
Jamaa: (Baada ya kugundua kampigia bisi wake akaa kimya....)
Bosi: "Nauliza hivi... Unajua unaongea na nani??!"
Jamaa (Kwa kuzuga ikabidi tu ajibu...): "Hapana..."
Bosi: "Mimi ni bosi wako humu ndani..."
Jamaa (Akakaza sauti na yeye): "Hivi na wewe unajua unaongea na nai??!"
Bosi: "Hapana, nani wewe?!"
Jamaa(Kwafuraha zaidi): "Daaaaah, asante MUNGU!!!!"
Then akakata simu!!!!!
0 comments: