Uzito wa mapenzi ni sawa na kilo 50 na maumivu yake ni sawa na kutembea na kilo 50 kwa umbali wa km5......soma

12:24:00 Unknown 0 Comments


Mama mmoja ambaye ni mfugaji wa kuku alienda duka la kununua chakula cha kuku na kuamua kumtafuta mtu mwenye toroli aweze kubeba.

Akamuuliza kijana mmoja kama anaweza kumtafutia mtu mwenye guta lenye uwezo wa kubeba chakula cha kuku chenye uzito wa kilo 50.

Yule kijana akajibu na kusema mimi hapa naweza tena kichwani bila hata ya toroli wala cha guta.

Mama akamwambia ila kumbuka ni uzito mkubwa kwa umbali tuendao wa kilomita 5, yule jamaa akamwambia achana na mimi mama, mimi nina nguvu wewe nipe mzigo.

Mama akamuuliza haya kwa umbali huu wa kilomota 5 na uzito huu wa kilo 50 utanichaji bei gani? jamaa akasema ni shillingi 2000 tu mama.Mama akamwambia haya beba twende.

Jamaa baada ya kuubeba ule mzigo na kutembea umbali wa zaidi ya mita mia, mzigo akaona unaanza kumuelemea na kwa ukali akamwambia mama yule, " wewe mama unaona huu mzigo unavyonitoa jasho????? sasa hutalipa 2000 ni 3000" kisha wakazidi kutembea na mama akiwa kimya.

Baada ya kumaliza kilomita moja tu jamaa akaaanza kunug'unika tena," mama wewe katili sana na walahuna ubinadamu huu sio mzigo wa kubeba binadamu bali punda sasa utalipa 5000"

Jamaa ali endelea kupiga kelele mpaka walipofika numbani kwa yule mama na bei bei ikawa imefika 20,000/= ingawa mama alimpaile ile ya mwanzo waliyo kubaliana kupeana na jamaa akaondoka kakasirika na ile 2000 yake huku akilia na kuanzia pale hataka tena kusikia kazi ya kubeba mizigo.

Funzo

Kijana huyu ni sawa na sisi tulio wengi ambao tunayakimbilia mahusiano bila ya kujua uzito wake na umbali tutakao safiri katika mahusiano yetu na maumivu ya mahusianao hayo.

Kabla ya kuingia katika mahusiano ni vyema kukaa chini na kufikiri ni kwanini tunahitaji kuingia katika mahusiano na mtu sahihi wa kuwa naye na kisha kuchukua maamuzi sahihi.

Ukishindwa kupata majibu hayo kaa kimya na usije kuwa mlalamishi kwa uzito wake na jifunze kwa mahusiano mengi ya sasa yanavyolipuka kama ugonjwa wa kipindupindi na kuwaachia wengi maumivu

Tafadhali tembelea na ku-like ukurasa wangu wa facebook kwa kubofya Nataka Kucheka

You Might Also Like

0 comments: