Vyakula vya watoto kuanzia miezi 6

12:37:00 Unknown 0 Comments

Hii makala inaendelea kutoka makala iliyopita. Ukitaka kuanza vizuri mwanzo tafadhali tembelea link hii: Fahamu juu ya lishe ya watoto.
Lishe ni msingi bora wa kumlea mtoto mwenye afya bora. Hii makala inalenga kukupa uelewa juu ya vyakula ambavyo mtoto anaweza kula ili kuwa na lishe bora, kuanzia miezi 6 hadi miaka 2. Hiki ndio kipindi muhimu kabisa katika ukuaji wa maisha ya binadamu.
Kwa mtoto anayeanza kula, ni muhimu apewe chakula kiasi kidogo ili kumfanya azoee. Si mara zote watoto hupenda vyakula mara ya kwanza, lakini baada ya muda huzoea na kukipenda.
Mtoto anayeanza kula apewe chakula laini kwa kipimo cha kijiko 1 mara 3 kwa siku. Kwa kila baada ya siku 3 hadi wiki endelea kuongeza idadi ya vijiko, wingi, uzito na aina ya chakula. Ni muhimu kutochanganya vitu vingi wakati mmoja, maana mtoto anaweza kupata allergy kutokana na vyakula na ukashindwa kuelewa nini kimesababisha.
Jinsi mtoto anavyozidi kukua boresha chakula chake taratibu kwa kutumia mafuta yenye afya, hasa yale yatokanayo na mimea mfano kweme, alizeti, mzaituni, nazi na maziwa. Vilevile, unaweza kutumia mafuta yatokanayo na viumbe wa baharini mfano, samaki.
Pia, ni muhimu mama ajitahidi kuhakikisha kuwa chakula cha mtoto kina virutubisho toka kwenye makundi yote 6 muhimu ya chakula– kabohadreti, mafuta, protini, vitamin, madini na maji.
Na kama nilivyogusia hapo awali, mtoto ale angalau mara 5 kwa siku kulingana na umri wake.

Lishe ya mtoto wa miezi 6

Kutokana na ushauri wa wataalamu wa lishe, mtoto mwenye miezi 6 huanza rasmi kupewa vyakula vya ziada huku akiendelea kupewa maziwa ya mama. Ni vizuri kuzingatia kuwa, mtoto anayeanza kula vyakula asimchanganyiwe vyakula tofauti muda wa mwanzo. Anza kumpa kitu kimoja kimoja ili kufahamu anapendelea vyakula gani zaidi na vipi hapendi. Mpe zaidi vyakula anavyopenda, huku ukiwa unamchanganyia vyakula asivyopendelea sana kwa kiasi kidogo. Hii itamfanya azoee vile vyakula asivyopenda na kuanza kuvipenda pia.
Kumpa mtoto chakula kimoja kimoja na kumsoma taratibu husaidia pia kufahamu vyakula ambavyo vinaweza kumletea mtoto madhara.
Vyakula vinavyoweza kuliwa kwa umri huu ni: uji laini, viazi (vizuri ukipata viazi lishe), mboga za majani zilizopikwa na kuiva vizuri na matunda yalivyopikwa, kuiva vizuri na kupondwa. Mfano wa vyakula na matunda ni boga, apples, ndizi, peasi.
Mtoto wa umri huu anatakiwa anyonye kwanza kabla ya kupewa vyakula vya ziada.  Vyakula vya ziada apewe mara 2 au 3 kwa siku na visizidi vijiko mpe 3 vya chakula.

Miezi 7 hadi 8

Mtoto mwenye umri huu anaweza kupewa vyakula mchanganyiko vilivyopondwa. Vyakula viwe na mchanganyiko wa makundi yote 6 ya vyakula. Ni muhimu pia kumpatia mtoto vyakula vya asili ya nyama (nchi kavu na habarini), matunda na mboga za majani.
Pia ni huu ni umri muafaka wa kuongeza aina moja mpya ya chakula kwa kila wiki. Muda wa wiki unatosha kukuonyesha kama mtoto anaweza kudhurika na chakula aina fulani. Jaribu kupunguza vyakula vyenye sukari nyingi. Sukari siyo nzuri sana kwa ukuaji wa mtoto, hasa ubongo.
Mtoto wa umri huu apewe chakula cha ziada mara 2 hadi 3 kwa siku, kwa idadi ya vijiko 3 hadi 9 vya chakula. Hii ikiwa ni baada ya maziwa ya mama.

Miezi 9 hadi 12

Mara nyingi watoto wengi wakifika umri huu huwa na meno na pia anakuwa anafahamu ladha ya vyakula mbalimbali. Hivyo, unaweza kumlisha vipande vidogo vidogo vya chakula vigumu au vyakula laini vilivyopondwa.
Katika vyakula vyake, unaweza kumpa matunda, na kuanza kumjaribu vitu mfano cheese, mboga za majani na vyakula jamii ya protini – nyama, samaki n.k.
Umri huu mtoto anaweza kupewa milo 3 hadi 4 ya chakula cha ziada kwa siku.
Kama mtoto anaweza kula kwa mikono yake, ni vizuri pia kumuacha aweze kujizoesha kuchukua vitu na kula, lakini fanya hivi mara baada ya kula kiasi kikubwa cha chakula alichotengewa. Watoto hupenda sana uhuru, wakati mwengine kumuacha ale mwenyewe huweza kumfanya ale zaidi ya kulishwa na mtu mzima.  
Ili kuweza kumfanya awe na uhuru wa kula, unaweza kutumia kikombe kidogo cha kulishia mtoto.

Miezi 12 hadi 24

Umri huu mara nyingi mtoto anakuwa anatembea, anaanza kuongea na pengine hata anaweza kuwa analazimisha zaidi kula mwenyewe. Ni umri unaoweza kuanza kumpa vipande vidogo vya chakula, hata vyakula vinavyoliwa na watu wazima. Ila kama bado hajaanza kula vizuri, unaweza kuponda chakula ili iwe rahisi kwake kula.
Pia, ni vizuri kumuanzishia vyakula tofauti kila baada ya wiki 1. Hii inaweza kumfanya azoee vyakula vingi zaidi na kumuanzishia tabia ya kupenda kula vyakula vya watu wazima.
Ni muhimu pia kuzingatia kuwa, mtoto anatakiwa kuendelea kunyonya hadi afikishe umri wa miezi 24, ingawa si mara nyingi kama ilivyokuwa wakati alipokuwa na miezi 6. Maziwa ya mama bado yana kazi muhimu kuboresha afya yake.

Je unafanyaje mtoto akikataa kula ?

Watoto hupita katika kipindi fulani huwa wanagoma kabisa kula. Ni kipindi kigumu kwa mzazi sababu mtoto anaweza kuwa na uzito mdogo na haongezei kama inavyotakiwa. Wengi huweza kupata vishawishi vya kumkaba mtoto ili ale, au kutumia nguvu na vitisho. Hiki ni kipindi cha mpito, na sababu za kukataa kula huweza kuwa :
  • Kumpa mtoto chakula, akiwa amechoka au ana usingizi.
  • Mtoto anayezoea kulazimishwa kula.
  • Kula ziadi vitu vyenye sukari nyingi kabla ya milo mikuu. Hii humuondolea hamu ya kula vyakula tofauti.
  • Mtoto akiwa hana njaa

You Might Also Like

0 comments: