Yametokea tena .........

12:39:00 Unknown 0 Comments

Yametokea tena .........
Nilishakataa katakata kuandika tena chochote juu ya maisha yangu na majanga yake ya kila siku na jamaa yangu mmoja ambaye jina sitamtaja maana mtamcheka.
Miezi kama minne iliyopita jamaa yangu alipigwa KIBUTI na binti aliyekuwa akipendana nae sana na walikaa kwa miaka kama minne hivi.
Ugomvi uliowafanya waachane ni kuwa jamaa alikuwa bado hajajiweka sawa kuoana na dada na dada yeye marafiki zake wote wameolewa na yeye sasa akawa na presha ya kutaka kuolewa.
Ugomvi ulidumu kwa muda huku jamaa akijaribu kumshawishi mamaa ili wavute subira lakini majadala huo ulifungwa baada ya kumshuhudia binti akitoka na jamaa mmoja hivi jina kapuni na sasa wako katika hatua za awali za maandalizi ya ndoa.
Jamaa yangu yeye akajikuta akiwa mtu wa bar na pombe kwa mawazo na hasikii lolote. Baada ya kumshauri sana aachane na hali hiyo basi bwana jamaa akaja na mkakati ambao ulikuwa kabambe.
Kuwa sasa alitaka kumtafuta binti mrembo kuliko yule binti wa awali na kuwa iwe ni bakora toosha kwa binti na kuona kuwa alisusa ambavyo bado vyapendwa na wengi.
Jamaa bwana kaja siku moja hivi na kuniambia amempata huyo binti na kuwa sasa niwe mpole atanifahamisha na tunatakiwa kupanga safari ya kwenda kumcheki huyo binti.
Kila siku jamaa alikuwa akija na picha mpya si whatsapp wala kwenye fb na kweli binti huyu mpya alikuwa matata ingawa hakutaka kuniambia yuko wapi najua labda ilikuwa ni hofu tuu akifiri kuibiwa.
Siku ikafika na akaniambia tunatakiwa kwenda tukuyu tukamchukue huyo binti na tutaenda mapaka matema na kukaa kwa siku chache huko yaani weekend ya jana.
Basi bwana tukatoka moja kwa moja na kagari ketu mpaka tukuyu, tumekaa sana pale stand wakiwasiliana kwa whatsapp lakini ikaonekna kama binti amebanwa hivyo tutangulie na jioni yeye ataingia.
Haikuwa mbaya sana tukaona ni vyema maana binti anadai ni meneja wa hoteli mija kubwa sana pale kyela na alikwenda tukuyu kikazi.
Tukafika matema na jamaa yangu akiwa na furaha ya kufa mtu tumeka ilipofikia saa nne kasoro jamaa nikaona kama anaishiwa pozi vile ingawa nikawa nimekudungua kuwa itakuwa ni kutokana na huyo mrembo kuchelewa.
Wakawasiliana na dakika chache akanifuta bar na kuniambia kuwa ametatua tatizo na binti yupo njiani anakuja. Tuliendelea kunywa huku tukimsubiri mpaka tunaenda kulala saa tisa kasoro mtu alikuwa hajaonekana.
Siku ya pili jamaa alijitahidi kutafuta kila njia ya kuwasiliana na yule binti lakini hakuna jipya lilotokea. Saa tisa na nusu ya jioni ndio tulijua kabisa kuwa tumeibiwa kwani yule mtu alimblock kwenye mitandao yote na ile namba ya whatsapp kumbe nayo ilisajiliwa kwa jina la kiume.
Jamaa ndio akaanza kuongea kumbe alishamtumia hela nyingi na binti kila muda alimuomba ampe namba ya wakala na jamaa atoe tuu.. na ndio kaibiwa tena.
kaibiwa mke, kaibiwa fedha lakini basi ndio tuaishi nafikiri alitakiwa atulie baada ya kuachika asilete ligi... haya ndio yaliotukuta weekend hii na mida hii ndio nawasili mbeya mjini
Like · Comment · 



Pata suruali kwa 25000 tu mawasiliano 0652192219
25000 tu mawasiliano 0652192219 Share
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: