" Ni wakati gani unamkumbuka Mungu wako?"

17:06:00 Unknown 0 Comments

" Ni wakati gani unamkumbuka Mungu wako?"

Msimamizi mmoja wa kamuni ya ujenzi ambayo imechukua tenda ya kujenga nyumba ya ghorofa yenye ghorofa 70 hapa jijini mbeya alikuwa juu kabisa ghorofa ya 10. ( achana na kuifikiri ghorofa hiyo iko wapi maana utaishia kuchanganyikiwa tuu kwani hakuna namna nyingine)

Akiwa ghorofani akawa anataka kuwasiliana na fundi aliyekuwa chini kwa kumpigia simu. Lakini kutoka na kelele nyingi pale chini yule fundi hakuisikia simu akawa busy na kazi yake.

Msimamizi akafikiria sana na kuona atumie njia mpya kwani alikuwa akimwona na hata kama angemwita asingemsikia pia. Basi akaingiza mkono mfukoni na kuitoa noti ya shilingi elfu 2 na kuitupa ishuke uelekeo wa yule fundi.

Ile noti ikaanguka pembeni ya fundi na fundi akaichukua na kuiweka mfukoni bila kuangalia juu na kuendelea na kazi. Jamaa kule juu akaona arushe tena noti ya shilingi 5000 lakini pia fundi akaichukua na kuiweka mfukoni bila kuangalia juu.

Jaribio hilo likawa limeshindikana hivyo akaona aje na wazo jipya.Akachukua jiwe dogo na kulirusha chini na likamgonga fundi yule mguuni. 

wakati huu fundi akaangalia juu na wakawasiliana na msimamizi wake.

Hadithi hii inafanana sana na maisha yetu, Mungu anatubariki kwa kutupa zawadi ndogo na kubwa katika maisha yetu lakini sisi tuko busy tunaendelea na mambo ya kidunia bila kupata muda wa kumshukuru au tukiendelea kutaka kupa zaidi kwa kuwa tunajiona wenye bahati.

Mungu anajaribu kutaka kuwasiliana nasi lakini sisi dunia inatupa presha na kutufanya tuwe busy na kumsahau kabisa...

Lakini Mungu anapoturushia jiwe dogo ambalo twaita matatizo hapo ndio tunakuwa na muda wa kuwasiliana nae na kuhitaji msaada wake tuondokane na shida hizo

Ndio maana nasema anatupa, anatupa na anatusamehe... na sisi tunapokea, tunapokea na tunamsahau......

Naishia hapa naelekea huko Karibu Mbeya​... nawe karibu

You Might Also Like

0 comments: