Kumpata rafiki utakayeendana naye bado ni kitendawili
Dan ni kijana mdogo mwenye umri wa mika 8, Lakini asubuhi hii dani anaonyesha uso usiona furaha huku akichukuliwa na basi la shule na uso wake haupo na tabasamu la kawaida.
Dan ni kama vijana wengine ambao wanahitaji kuwa na ndoto nzuri za hapo baadae na kufurahia utoto hasa akipewa nafasi ya kucheza na midori pamoja na kula vitu vizuri, lakini yeye hapati muda huo kwani usiku na mchana anakerwa na sauti za hasira za baba na mama wakigombana.
Siku ya pili anaenda shule tena na kurudi kukuta hali ileile kama kila siku anavyoacha baba na mama wakipigana na hata kukosa kupata nafasi ya kukaa na kufurahia uwepo wao katika maisha yake.
Dan anakimbia na kwenda kujifungia chumbani analia sana na kuomba Mungu baba na mama wapotee asiwaone kabisa kwani anachoshwa na nyumba yao kutokuwa na amani.
Lakini anafikiria kwa kina na baadae anaamua kulia na kubaki kama alivyo kwani anaamini kila atakaloliomba sasa laweza kuja mfanya ajute hapo baadae katika maisha yake. Anaamini kuwa pamoja na kuwa baba na mama wameona lakini bado sio marafiki wanaofanana.
Dani anachukua daftari lake na kuandika " Utamchagua rafiki ila kamwe hutampata rafiki mtakaye endana hivyo ni vyema kujifunza kuishi na watu tulionao"
Funzo
*Kumpata rafiki mtakayeendana naye ni kazi ngumu
*Watoto wetu hujifunza mengi kutokana na sisi wazazi tunavyoishi
*Jambo unaloliomba au kulifanya sasa laweza kuja kukudhuru hapo baadae
*Ni vyema kuyatafakari maisha yetu kabla ya kuchukua maamuzi juu ya wengine
* Ni vyema kujifunza kuishi na watu tulionao

0 comments: