Mfalme asiyekuwa na Jicho moja na Mguu mmoja

02:49:00 Unknown 0 Comments

Hapo zamani kulikuwa na mfalme aliyekuwa hana jicho moja na mguu mmoja.....

Siku moja akawakusanya wachoraji wote pale nchini kwake na kuwa ambia wachore picha nzuri ya yeye...Lakini wale wachoraji wote wakashindwa  kuichora-- Wangewezaje kuichora picha nzuri wakati mfalme ana kasoro katika jicho na mkuu?

Lakini kwa bahati nzuri mmoja kati ya wachoraji wale akaamua ajitose na kuchora picha ya mfalme.


Ilikuwa ni picha nzuri iliyomshangaza kila mtu pamoja na wachoraji wenzake....

Alischora picha Nzuri ikimwonyesha mfalme anataka kuwinda na jicho moja kalifunga na jingine kaliweka kwenye lensi ya bunduki na mguu mmoja ameukunja

Funzo 
:

Kwa nini tusichore picha kamahizi kwa wengine.Kuficha mapungufu ya wenzetu na kuonyesha mema yao.

Wengi tumekuwa wepesi wa kuonyesha madhaifu ya wenzetu kuliko mazuri yao


You Might Also Like

0 comments: