Naweza kuwa nachezewa au binti kapatwa na matatizo??
Hello Fuledi,
Mimini kijana wa miaka 34 ni mfanya biashara ila sijabahatika kuwa na mchumba.
Hivi karibuni nilimpata binti mmoja ambaye anaishi katika kambi za wakimbizi huko Senegal na familia yake waliuawa huko wakati wa machafuko na kuacha hela nyingi ambazo ziko benki na yule binti hawezi kuzitoa kwani yupo kambini.
Dada akaniomba nimsaidie ili nizitoe nikishirikiana na wakili wake na kiasi cha pesa nichukue na kidogo apewe yeye na wakili wa baba yake na kiasi kitakachobaki tupeleke kwenye vituo vya watoto yatima.
Kwa kuwa hakuwa na hela ikanibidi nitafute hela na kuanza kumsaidia mchakato na kuwasiliana na wakili wake na kutuma fedha na mambo yakawa safi.
Mpaka sasa nimeshatumia hela nyingi na sasa si cha wakili wala yeye hawapatikani wakati hela ilibidi niingiziwe tangu mwezi june.
Naweza kuwa nachezewa au binti kapatwa na matatizo??
Naombeni msaada wenu marafiki
0 comments: