Nanihii imeanza kuwa na majanga

01:22:00 Unknown 0 Comments

Sikuwahi kufikiria kuwa kuna siku ningeweza kuaibika kisa mimi mwizi,lakini tamaa imeniponza.

Nilihitimu chuo cha ufundi stadi miaka kadhaa iliyopita, lakini nikajikuta nikiwa na uzoefu mkubwa wa kukaa mtaani na kuomba kazi bila mafanikio.

Nilianza pata tetesi za fulani kanunua verosa, nani hii kanunua alteeza na yule demu mfupi mbaya kanunua RAV4 na Joshua sasa ni meneja wa ofisi fulani.

Kweli maneno hayoyalianza kunipa wazimu na kukumbuka jinsi nilivyokuwa nikionekana maridadi pale shuleni hasa kwa kuvaa sura ya maisha ya juu wakati ukweli ulikuwa na mimi mwenyewe.

baada ya kupata yale maneno kiukweli hasira ya kuwa na gari na maisha mazuri ikanipanda, Nakumbka jumapili moja rafiki yangu mmoja akanifuata na kuniambia kuna deal moja tamu sana kweli tukaenda na kumkaba jamaa na kisha kumwibia milioni saba na laki kadhaa kwani tulipata habari kuwa alikuwa na hela keshi za kununulia miti ya mbao.Mgao ule ndio ukanipa hamasa ya kuendesha gari langu.

Wiki tatu zilizopita nilienda kwa mzee mmoja ambaye sasa baada ya mkasa ndio nakuja kugundua ni mwenyeji wa sumbawanga.

Yeye tulienda na kumwibia kuku 456 wa nyama katika banda lake na kwenda kuuza. Mzee alibandika matangazo kuwa aliyeiba kuku wake aende akajisalimishe lakini mie nikaona sio.

Siku ya nne leo nimeona nikajisalimishe kituo kidogo cha polisi kwani tumboni kuna vitu vya ajabu na mbaya sana ni kuwa baadhi ya viungo vyangu vya mwili kila baada ya dakika kadhaa vinabadilika na kuwa na maumbo tofauti.

Kilichonitisha zaidi ni baada ya nanini hii yangu kubadilika na kuwa na umbo la ajabu na sasa nimejisalimisha mwenyewe. kwa mzee na kituoni lakini mzee hataki kuonyesha dalili ya kunielewa. na sijui mwisho wangu ni nini.

Ndugu zangu maisha haya hayahitaji pupa naishia hapa kwa muda

Niombeeni

You Might Also Like

0 comments: