“Nitasema maneno yaliyopo kwenye kitabu kitakatifu “
Daktari mmoja aitwaye
Fuledi aliingia hospital kwa haraka baada ya kupigiwa simu kuwa alitakiwa kwa ajili ya operesheni ya haraka
sana.Moja kwa moja bila kupoteza muda Dr Fuledi aliingia katika chumba cha
upasuaji.
Akamwona baba wa kijana
aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji akiwa katika chumba cha kusubiria.
Baada
ya kumwona Dr Fuledi baba wa kijana alipiga kelele huku akimfuata na
kumwambia: “Kwa nini umechukua muda mrefu
kuja? Haujui kuwa motto wangu angeweza kufa? Una chembe ya ubinadamu wewe au
kwako vifo ni ufahari?”
Fuledi
alitabasamu na kumwambia Yule baba: “Sikuwa
hapa hospital ila baada ya kupigiwa simu nimekuja haraka kama nilivyoweza……
Nakuomba samahani na uwe mpole nifanye kazi mara moja”
“Niwe mpole?! Ungekuwa wewe
ndio mimi na mototo wako anataka kufa na daktari anakuambia uwe mpole ungekuwa
mpole? Aliongea baba Yule akiwa na hasira za kutisha.
Daktari
Fuledi alitabasamu tena na kumjibu mzee
yule: “Nitasema maneno yaliyopo kwenye kitabu kitakatifu “Tuliumbwa
kwa mavumbi na tutarudi mavumbini, Jina la bwana libarikiwe”. Daktari hawezi
kurudisha Maisha ya mtu bali kwa neema zake bwana. Mwanao atapona kwa jina la bwana.
“Huwezi kunipa ushauri wakati wewe sio mwajibikaji hivyo huna
maana” Aliongea baba kwa hasira
Upasuaji
ulichukua masaa kadhaa na baadae daktari Fuledi akafungua mlango na kutoka
akiwa na uso wenye furaha na kumwambia baba “Ashukuriwe Mungu mtoto wako kapona na bila kupoteza muda Fuledi akaondoka kabla
ya Yule mzee hajadadisi zaidi.
Mbona huyu daktari mkorofi sana, yaani hata kabla sijamaliza kuuliza
kaondoka? Aliuliza yule mzee kwa nesi
aliyekuwa pembeni yake.
Nesi
akamjibu huku machozi yakimtoka: “ Mtoto wa daktari huyu alipata ajali na kufa
jana, Alikuwa nyumbani akijiandaa kwenda kumzika,Na kwa kuwa hakuna daktari wa
tatizo hilo zaidi yake basi tukampigia
ndio akaja mara moja na sasa anawahi kwenda kumzika mwanae.”
Funzo :
Usiwe mwepesi wa kuhukumu….. kwa sababu huwezi jua wenzako ni kwa
nini wako na hali unazoziona zikiwaandama au watu wanapitia Maisha ya namna
gani wakijitahidi kukufanya wewe uwe na furaha na amani.
0 comments: