Tembo aliyefunzwa

18:42:00 Unknown 0 Comments



Siku moja Fuledi alikuwa akipita karibia na Zoo, kwa bahati mbaya akamwona tembo mkubwa akiwa mbele yake akaogopa kupita na wakati akiendelea kumwangalia akaona kafungwa na kamba ndogo ambayo angeweza kuiata kutokana na ukubwa wake.

Pembeni kidogo kulikuwa na mtu mmoja ambaye ndio mwalimu wa tembo yule katika zoo ile, Mwalimu akamuuliza Fuledi mbona umeshtuka? Huyo hawezi kukudhuru kwani kaizoea hiyo kamba.

Fuledi kwa mshangao akauliza "inakuaje asikate wakati ni mkubwa sana huyu tembo na ananguvu?" Yule jmwalimu akasema kuwa "tumewafundisha tangia wakiwa wadogo kwa kuwafunga kamba hiyo na sasa wakiwa wakubwa huamini bado kamba hiyo ina nguvu hivyo hawawezi kudhuru watu wakiogopa kamba hiyo kuwa itambana".

Fuledi alishangaa sana kwani kwa ukubwa wa tembo yule angeweza kuikata kamba muda wowote ule ila wamefundishwa kubakia na imani ya kuwa hawezi kuikata kamba yaani bado wana imani ya utoto wao wakati kamba ile ilivyowazuia kuwa huru.

Kama ilivyo kwa tembo ni watu wangapi tumeendelea kuishi maisha ya kuamini kuwa kamwe hatutafanikiwa jambo fulani kwa kuwa tuliwahi kushindwa mwanzoni?

Funzo

Kushindwa ni moja ya njia ya kujifunza. Hatutakiwi kukata tamaa katika kila jambo tufanyalo, leo utashindwa ila kesho jaribu tena na utafanikiwa kwa sababu wewe ni mfano wa mafanikio utakayo na unatakiwa kujifunza kila siku katika maisha yako kupitia kushindwa.

powered by www.tabasamunafuledi.com

You Might Also Like

0 comments: