TIGO EXPESS YOURSELF

08:01:00 Unknown 0 Comments

Jamaa mmoja alikuwa na hisia za
kimapenzi kwa dada fulani mda
mrefu sana ila hakuwa na moyo wa
kujieleza..
Usiku mmoja aliamua kujikakamua
na kutoa simu yake akamtumia binti
sms..'' i love u so much, tafadhali
nijibu hisia zako ''
baada mda mchache simu yake
ikapokea reply, KARIM aliishiwa
nguvu kwa wasiwasi wa kutaka kujua
binti amejibu nini, akaamua kulala
aisome sms siku inayofwata labda
angekuwa na ujasiri wa kuifungua
msg hiyo.
Siku ilofwata asubuhi KARIM aliamka
mapema na kufanya usafi wa
nyumba na kazi zingine, mwisho
akapata mda wa kukoga na ndipo
akarudi kitandani kwa ujasiri ili
asome alichojibiwa..
Kufungua sms akakuta...
'' hauna salio la kutosha kutumia
huduma hii, bonyeza *149*22#
kupata tigo niwezeshe. TIGO EXPESS
YOURSELF ''

You Might Also Like

0 comments: